Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3.Jizoeshe kuwa na utulivu.

Acha kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja. Fanya kitu ambacho kinaleta mabadiliko kwenye maisha yako kwa muda wa kutosha. penda utulivu. furahia kila unachokifanya mkononi mwako, na utambue ubora wa hicho kitu unachokifanya.
 
C51E5653-956F-4D4B-BEF3-B151CD81576D.jpeg
 
4.Jijengee Furaha, Amani .



Pata Nuru ya uchangamfu, ukichagua furaha na amani utapata upendo. Kila changamoto itakuwa ni ndogo kwako. Angalia wakati ambapo unaweza kuwa mchangamfu kitu gani huwa kinatokea, tambua ni jinsi gani mwili huwa unarelax, pumzi zako na akili yako. ni zoezi rahisi lakini linakupa mafanikio makubwa na ya miujiza mikubwa.
 
5.Kuwa mtu wa Shukurani.

Shukuru kwa kila jambo. liwe zuri au baya. unaweza ukakutana na vipengele vigumu kwenye maisha yako, na ukasahau kushukuru jinsi gani kila kitu Mungu amekiweka kiwe hivyo.Shukurani inaweza kuwa ni zoezi zuri, litakusaidia kuwa na upole na kutambua nyakati mbalimbali katika maisha. Sema asante kwa afya uliyonayo, kwa wema Mungu anaokutendea, Kwa uzuri wa hali ya hewa.
 
Zoezi hili litakuwa rahisi kwako kama utaanza kumkumbuka Mungu kila ikifika saa kamili. haya ni mashariti madogo, kuliko kama ungeenda kwa mganga wa kienyeji. Achana na maombi ya kulalamika, kusikitika, kusononeka, kulaumu, kusema Mungu mbona mimi, Mbona umeniacha.
 
Anza leo zoezi la kumkumbuka Mungu kila inapofika saa kamili ili akupe nguvu ya kujenga sifa ya ndani yako . sifa hio ndio ambayo itakusaidia wewe katika kila sekta ya maisha yako. Mpe Mungu dakika moja tu kwa kila dakika 60. ni mbegu unapanda.
 
Omba Mungu akupe Roho ya Hekima, Maarifa , Uweza,Ufahamu , Roho ya Ushauri, Roho ya kumcha yeye. Muombe MUngu akusaidie uwe na Upendo , Amani, Utu wema , Fadhili, Uaminifu, Upole, Uvumilivu, Nidhamu ya Muda, Na uwe na kiasi kwa kila unachokifanya. Hakuna mahali utashindwa endapo ndani yako utakuwa na sifa hizi. Ukitumia muda vizuri hutatenda dhambi.
 
Hakuna kitu ambacho kinakuja kwa urahisi maishani kinachoweza kudumu. Lazima ufanyie kazi kwa bidii ndipo utapata kitu cha kudumu. kwa hio anza leo. Mkumbuke Mungu, Msifu Mungu, Mshukuru Mungu kwa kila kitu .Kila inapofika saa kamili mpe Mungu dakika moja tu, msifu, mshukuru. uwe mtu wa toba kila mara.
 
Back
Top Bottom