Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

5.Picha na Kichwa cha habari yako kiendane na ulichoandika kwenye post yako. Vinginevyo utapata watu wengi kwa wakati mmoja, na hakuna atakaerudi kwako tena kwani hakupata alichokifuata. Haina faida kupata watu elfu kumi leo, halafu kesho usipoandika chochote unapata watu watano!
 
G'morning madame
 
6. Blog za habari na udaku ndizo zenye wafuatiliaji wengi zaidi hasa kwa nchi yetu, Hivyo kama unaamua kufungua blog ya habari au udaku, hakikisha una watu wanaokutafutia habari kona zote, usitegemee kunakiri kwa mtu mwingine kila siku kwani utajikuta unaonekana wewe ni mfuasi wa wenzio na si mshindani.
 
7.Usikimbilie kuweka Matangazo ua “adsense” au “adwords” kwani huwaudhi watembeleaji na blog yako haitakuwa na mashabiki na hivyo, haitadumu muda mrefu. Weka Matangazo haya baada ya kukua vyakutosha na unauhakika wa kundi kubwa nyuma yako.
 
8.Usiweke Pesa mbele, hakikisha kwanza blog yako inataarifa za kutosha kuhusu unachokiandika, Itakulipa baadae sana baada ya kuaminiwa na watu. Ukitaka fedha nyingi kutoka kwenye blog, hakikisha unawekeza kwenye blog hiyo kwa kuitangaza.
 
10.Linalobeba yote katika suala la kuamua kuwa na blog ni neno UVUMILIVU. Kwanza utaonekana umekosa cha kufanya, kuna kipindi watu hawatakuunga mkono kabisa, baadae unaweza kukata tama baada ya kuona kiasi cha ushindani ni kikubwa sana! Unatakiwa usiwe na haraka, jaribu kutengeneza blog leo, hakikisha unakuwa na kiyu kipya kila siku bila kukata tamaa kwa mwaka mzima bila kujali unapata watu wangapi, baadae itakulipa tu! Usiwe na shaka..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…