Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili ilipoanzia hadi sehemu nyingine huitwa metastatic cancer na tendo la kansa kuenea kutoka sehemu moja hadi sehemu nyingine ya mwili huitwa metastasis. Kansa iliyoenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi sehemu nyingine huwa na aina ya seli zilezile za sehemu ambako ilitokea na hupewa jina lile lile la aina ya kansa ya sehemu ya mwanzo ilikotokea. Kwa mfano,
 
28766021_184034499051735_6318748545776091136_n.jpg
 
kansa ya ziwa iliyoenea na kwenda kujenga uvimbe katika mapafu haitaitwa kansa ya mapafu bali metastatic cancer ya ziwa na uchunguzi kwa vyombo maalumu wa seli za sehemu hizi mbili utaonyesha kufanana kwa seli za sehemu hizo mbili toauti. Kansa hizi zinazotokea kwa kuenea kutoka sehemu moja ya mwili hadi nyingine (metastatic cancers) huleta madhara makubwa kwa ufanyaji kazi wa mwili na idadi kubwa ya watu
wanaofariki kwa saratani, hufariki kwa sababu ya aina hii ya kansa.
 
Aina Za Kansa



Mara nyingi aina za kansa hutajwa kutokana na kiungo ambako kansa hiyo ilianzia. Kwa mfano, kansa iliyoanzia kwenye mapafu itaitwa kansa ya mapafu na ile iliyoanzaia kwenye ubongo itaitwa kansa ya ubongo. Kuna namna nyingine za kuzitofautisha kansa, kama vile kwa kutaja aina ya seli zilizozijenga kansa hizo.
 
Hapa chini ni baadhi ya makundi ya kansa zilizoanzia kwenye aina fulani ya seli:

Carcinoma
Carcinomas ndizo kansa zinazoshambulia zaidi watu kuliko aina nyingine zote za kansa. Kansa hizi zinajengwa na seli zinazofunika maeneo ya ndani na ya nje ya mwili (epithelial cells) ambazo zipo za
aina nyingi.
 
Carcinoma hupewa majina kutokana na aina ya seli zilipoanzia:

Adenocarcinoma ni kansa zinajojenga seli za epithelial zinazozalisha majimaji au ute. Kansa nyingi za maziwa, utumbo na tezi kuu huwa ni za aina hii (adenocarcinomas).
 
Basal cell carcinoma ni aina ya kansa inayoanzia kwenye tabaka la chini la epidermis – epidermis ni sehemu ya juu ya ngozi ya mwili.
 
Squamous cell carcinoma ni kansa inayojenga kwenye seli ziitwazo squamous cells – ambazo ni seli za epithelial zilizo chini ya ngozi mara baada ya sehemu ya juu kabisa ya ngozi. seli za Squamous pia hufunika viungo vingine vingi vya mwili ikiwa ni pamoja na tumbo, utumbo, mapafu, kibofu cha mkojo na figo. Kansa za aina hii pia huitwa epidermoid carcinomas.
 
Pia kuna aina ya kansa iitwayo Transitional cell carcinoma ambayo hushambulia ngozi inayofunika kibofu cha mkojo, ureters, sehemu za figo na maeneo mengine.
 
Sarcoma
Kundi hili la kansa linajumuisha saratani zinazojenga kwenye mifupa na sehemu laini za amwili kama kwenye misuli, mafuta, mishipa ya damu. mishipa ya lymph, tendons na ligaments.
 
Sarcoma
Kundi hili la kansa linajumuisha saratani zinazojenga kwenye mifupa na sehemu laini za amwili kama kwenye misuli, mafuta, mishipa ya damu. mishipa ya lymph, tendons na ligaments.
 
Katika kansa za mifupa osteosarcoma ndiyo inayoshambulia idadi kubwa zaidi ya watu. Osteosarcoma huanzia kwenye seli za kuzalisha mifupa mipya (osteoblasts) na ni aina saratani amabya hushambulia zaidi vijana wa umri mdogo. Saratani hii mara nyngi hujenga sehemu inapoishia mifupa mirefu ya mwili ambayo ni mifupa ya mikono na miguu. Kwa watoto wachanga na wale wa umri wa zaidi ya miaka kumi, hujenga zaidi karibu na magoti.
 
Dalili kuu za osteosarcoma ni uvimbe kwenye eneo la mfupa, maumivu kwenye mfupa au joint na kuvunjika kwa mfupa kusikoambatana na sababu yo yote ile. Kansa hii huchochewa na tiba ya mionzi na matumizi ya vidonge vya kuzuia kansa vinavyoitwa alkylating agents.
 
Back
Top Bottom