Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

USIKIMBILIE KUWA MZAZI YAJUE HAYA KUMI MUHIMU KWANZA.

1.Maisha yako yatabadilika moja kwa moja! Utajifunza matumizi mazuri ya fedha, ulaji, kuendesha gari kwa hekima, Mahusiano na mpenzi wako yatabadilika (kwa uzuri au ubaya) mtajiona wa tofauti sana. Muda wako wa ziada utapenda ulale kwani kukosa usingizi halitakuwa jambo la ajabu.
 
2.Utatakiwa upende anachopenda Mtoto.
Sahau kuhusu timu yako uipendayo kwa muda, kipindi chako ukipendacho, utajua machache sana yanayoendelea duniani, na sasa utapenda anachopenda mtoto. Utakuwa mtoto kwa muda, hii ni kawaida sana.
 
3.Nyumbani Kwako kutakuwa kijalala Kidogo
Watoto wanapenda michezo mingi sana! Usitegemee kukuta sebule yako ni safi muda wote kama ulivyozoea, usifikirie kwamba atavijali vitu vyako kama unavyojali wewe.
 
4. Simu/ Computer yako itakuwa ya mwanao.
Licha ya juhudi zote jua ya kwamba watoto watagusa simu, au computer yako tu! Watapenda kuwa na wewe, kufanya kazi kama wewe, na kutumia vitu vyako. Hakikisha vitu vilivyo kwenye simu, au computer yako vinamfaa, na hakuna ubaya akiona.
 
Back
Top Bottom