3. Wajua wavuta sigara wana hasira za haraka? Baada tu ya masaa 24 yaani siku moja baada ya kuacha sigara, mvutaji hujisikia mwenye amani na akikaa hivyo kwa wiki moja zaidi hujisikia katika hali bora zaidi.
4. baada ya siku mbili tu toka uache kuvuta sigara, neva zilizoanza kufa huanza kurudi katika hali yake na kiwango cha kunusa na uwezo wa ulimi kutambua ladha huongezeka
Siku tatu baadae mwili wako hautajisikia kuwa na nicotine tena kwa asilimia 100% japo bado itakuwepo kwa kiasi Fulani. Na utaanza kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa kama TB au mshtuko wa moyo.
Wiki moja tu baada ya kuacha sigara utakuwa na uwezo wa kufanya shughuli yoyote ya kutumia nguvu ambayo mwanzo ulikuwa ukichoka kwa haraka baada tu ya kufanya hivyo.
Miaka mitano baada ya kuacha sigara Utakuwa umepunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupata kiharusi. Na kupunguza kama si kuondoa kabisa uwezekano wa kupata TB (inategemeana umevuta kwa mda gani)
10. Miaka Kumi na zaidi baada ya kuacha sigara, tapunguza uwezekano wa kupata kansa ya mapafu, na madhara hayataonekana mwilini mwako kwa asilimia karibu mia moja (100%) na Utakuwa na furaha zaidi maishani.