Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mimi ni nani?

Kwa nini nipo Ulimwenguni?

Naenda Wapi?

Zaidi ya hayo, Nilitaka kuwa huru.Nilitaka uhuru kama wengine walivyo huru. Kila mtu anaweza kufanya hivyo. Uhuru wangu ulikuwa kufanya kitu ambacho hata watu hawajakifanya kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Kwa hio nilianza kutafuta majibu.
 
Ni wapi Unaweza kupata mabadiliko ya kweli?

Ilionekana kuwa kila mtu anakuambia kuwa ni kwenye dini tu. huko ndio utapata majibu ya kweli
 
Wakati mwingine nikifikiria maisha naona kama hayana sababu. Usihamaki lakini.Wazo lote hili la kusudi la maisha naona kama sio sahihi. Haya ni mawazo yangu.– maisha huwa yanakuja kama na uchoyo
 
Wakati mwingine nikifikiria maisha naona kama hayana sababu. Usihamaki lakini.Wazo lote hili la kusudi la maisha naona kama sio sahihi. Haya ni mawazo yangu.– maisha huwa yanakuja kama na uchoyo
 
Maisha siku zote yanatakiwa yawe ya furaha, kucheza, kuwa na amani, yawe na ucheshi, bila ya kusudi lolote. Maisha yana mwisho wake , hayana mwisho wa kingine. Wakati utakapoelewa hivyo, utaelewa maana ya utulivu wa akili kwa kutumia meditation
 
Ni kuishi maisha yako kwa kufurahia, bila ya sababu yoyote ile. Furaha tu bila kusudi lolote, bila mtazamo, yasiwe na kusudi hata kidogo. Yawe tu kama watoto wadogo ambao wanacheza kwa kukusanye mawe na mchanga na kujenga nyumba — kwa ajili ya lengo gani?
 
Karne nyingi zimepita , watu wakijaribu kuwa watakatifu kila siku, hakuna hata aliyeona mwisho, wengine wanaamua kuishi msituni bila ya kula , hakuna chai wala kahawa, hakuna mikate, hakuna taarifa yoyote wanayopata, Hakuna wanachokipata. Hakuna mwenye kuona ukweli wa maisha . wengine wanaamua kujichoma moto. Hio yote ni kutafuta furaha ya maisha, na kutaka kuwa watakatifu..Hio ni ngumu .
 
Unaweza kujaribu kwa muda wa miaka mingi, kutafuta kichwani mwako na nje yako kila mbinu , kufanya kila aina ya vitu, lakini hutaweza kuona kwa sababu hio sio sehemu ya kitu kilichopo . kwa hio uwe makini , kabla hujaanza kutafuta kitu ambacho umekipoteza mkononi mwako . usiwe na haraka. Jitengeneze kwanza moyo wako.
 
Ishi wakati uliopo, wakati uliopo ndio unatengeneza wakati ujao, na utakuwa mwenye furaha na utulivu. Fanya tafakari, fanya mazoezi, fanya kazi unayoipenda, lisha moyo wako, lisha akili yako kwa kutafuta ufahamu, jipende, jikubali, jiheshimu, jijali mwenyewe.
 
Kinyume cha haya ni kukosa ujasiri, thamani, ukweli wako. na utapungukiwa na self-esteem kutokana na kutoelewa watu wengine.

Kumbuka kukosa uelewa ni kupoteza thamani ya maisha yako.
 
Back
Top Bottom