Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kati ya wanyama hao ni wawili tuu ndio hupata bahati ya kuwala twiga wakubwa nao ni chui na mamba, bahati waliyonayo ni kwamba chui humkamata Twiga anapokula majani katika mti aliopo na mamba humkamata anapokunywa maji, waliosaria huishia kuwinda watoto wa twiga tuu.
 
Kati ya wanyama hao ni wawili tuu ndio hupata bahati ya kuwala twiga wakubwa nao ni chui na mamba, bahati waliyonayo ni kwamba chui humkamata Twiga anapokula majani katika mti aliopo na mamba humkamata anapokunywa maji, waliosaria huishia kuwinda watoto wa twiga tuu.
 
Kiumbe huyu ana ulimi mrefu sana, humsaidia kula majani ambayo yamemea katika miti yenye miba, ni mnyama anayehusudu sana misosi anaweza kula hadi kilo 50 na ushee, pia ni wanyama ambao hawaamini katika kuishi katika mipaka, kwa lugha nyepesi ni mnyama anayeishi kwa kuhama hama na hii ni kutokana na kutafuta chakula kwani hutumia chakula kingi sana, hasumbuliwi sana na kiu, hivyo maji sio ishu sana ikiwa kama atapata majani yenye unyevu nyevu.
 
Ni mnyama mpole anayeamini sana katika amani, ila hataki kabisa kusikia mambo ya kuonewa na huwa haogopi kitu, na wakati mwingine huamua kukimbia ili kuepusha Shari hata kama lililopo mbele yake analimudu, ana ustarabu uliotukuka.
 
Muone mwembamba vile vile lakini ni mzito sana, ana kilo zaidi ya 500 na kadri anavozidi kukua hufika hadi 800 kg, umri wake wa kuishi ni miaka 25 tuu, ambapo kama atafikisha umri huo basi atakufa kwa uzee au kukamatwa kizembe na chui au mamba.
 
Ukiwaona unaweza kuwatofautisha kwa kuwatizama kichwani, Dume huwa na pembe fupi sana ambazo unaweza usizione kama hautakuwa makini kwani huwa na urefu wa nchi tano tuu, na jike hukosa kabisa au huchomoza kidogo sana kutokana na umri.
 
Twiga ni mnyama mrembo mbali na kuwa na haiba ya kuvutia kwa urefu wake, lakini pia ana ngozi yenye rangi nzuri, macho yake ni makubwa na anajua kuyatumia vyema kutizama jambo ambalo humuongezea sifa, katika umri wake wa miaka mitano huwa tayari amepevuka na yupo tayari kwa kumjua dume, na dume huwatambua kwa kutizama mkojo wake tuu, mnyama huyu ana uwezo mzuri wa kukimbia ila ni miongoni mwa wanyama ambao wanajichochea yaani kwa kadri anavyokimbia ndivyo spidi yake inaongezeka wenzie wenye sifa hiyo ni pamoja na mbuni, tembo nk.
 
Ni mnyama mrefu kuliko wote waishio ardhini.
2. Ni mpenda amani sana.
3. Ni mnyama ambaye wanyama wenzie wanaokula majani hujisikia amani sana kukaa naye kwakuwa huona hatari tangu ikiwa mbali, sasa usishangae akina pimbi swala wakijaa chini yake.
 
Back
Top Bottom