Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji23]
IMG_20180408_204645_140.jpg
 
Una habari kwamba brooklyn beckham (15), mtoto wa bilionea na mwanasoka wa zamani maarufu duniani David Beckam anafanya kazi mgahawani? Tena analipwa euro 2.6 kwa saa Yaani Sh 6000/= za kitanzania.
 
Je baba yake asingeweza kumpa mshahara mara 10 ya huo tena kwa kukaa tu ndani?. Utakubaliana na mimi kwamba wazazi wa sasa wanawekeza zaidi katika maisha ya watoto wao kuliko kizazi chochote kile kilichowahi kutokea! Pengine ni mabadiliko ya kimaisha, lakini Je, hiki tunachokiita “malezi ya kisasa” Kinaweza kuleta Madhara gani Baadae? Je, tunatengeneza taifa la namna gani baadae? Nia yangu sio kumnyooshea mtu kidole bali kujaribu kujenga uelewa zaidi katika jamii yafuatayo ni baadhi ya mambo kumi wazazi hukosea katika malezi:
 
1.Tunalea “Mtoto tunayemtaka” sio “mtoto tuliyenae”
Wazazi wengi hulea watoto wao wakitaka kuwachagulia aina Fulani ya maisha bila kujali mtoto walienae anaweza vitu ganina na kupenda nini. Badala yake kila mzazi huamini mwanae atakua na tabia kama za kwake na pengine atakua na akili na uwezo zaidi au hulazimisha mwanae awe na kipaji Fulani eti tu kawa kuwa mzazi ana kipaji/kalama hiyo! Kumbe ingekuwa hivyo basi tusingehangaika kutafuta viongozi, wanasoka au wasanii bora kwani tungewatumia watoto wao tu!
 
Kusahau Kuwa Vitendo vyetu (wazazi) vinaongea kwa sauti kubwa zaidi ya maneno/ nasaha zetu
Unaishi vipi na majirani zako? Je unaishi vipi na mwenzi wako hapo ndani? Unaishi vipi na wageni? Kama ulikuwa hujajua, basi tambua kwamba mwalimu wa kwanza wa mtoto ni mzazi, mtoto yeyote anapokuwa hupenda kuwa kama baba/mama yake. Je anayoyaona unayafanya ni sawa na unachomwambia afanye?
 
Kudharau Tabia za mwanzo za mtoto
Tabia yoyote anayokuonyesha mwanao katika umri mdogo, ndiyo hiyo atakayoionyesha akiwa na miaka 30!. Kama anatabia ya ubinafsi, ambayo pengine kajifunza kwa mzazi mmojawapo, shuleni nk, basi usitegemee maajabu kuwa mtoto atabadilika na kutumia neno “ni utoto”. Zijue tabia Za mwanzo za mwanao, mbadilishe mapema iwezekanavyo (kama ni mbaya) kwani akizoea itakuwa sehemu ya maisha yake na itakuwa “vita” kutaka kumbadilisha akiwa na umri mkubwa zaidi.
 
Back
Top Bottom