Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

MAGONJWA YA KIFUA:

Damu kuvilia kwenye mapafu
(Pulmonary Embolism)
 Damu kuvilia kwenye mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary embolism)
 Vijidudu kwenye mapafu – husababisha homa ya vichomi (Pneumonia, Bronchitis, Tuberculosis/TB,) n.k.
 
Kujaa maji, damu au hewa kwenye mfuko wa nje wa mapafu (pneumothorax, haemothorax or pleura effusion)
 Saratani
Picha inayoonyesha damu iliyovilia kwenye mapafu (Pulmonary embolism)
 
Dalili:
 Haya husababisha maumivu ya kifua aina ya vichomi,
 Au maumivu makali wakati wa kupumua – kuvuta hewa
 Maumivu huwa popote katika kifua, bila kusikika nje ya kifua kama kwenye bega au shingo (non radiating type)
 
Husababisha shida katika kupumua, mtu kujisikia kukosa hewa na kuhema haraka haraka
 Mara nyingine husababisha rangi ya midomo au mikono kubadilika kuwa blue(cyanosis)
 Homa au kutoka jasho sana hasa wakati wa usiku huashiria vijidudu – virusi, bacteria, TB nk.
 Mara nyingi huambatana na kikohozi – kikavu au chenye makohozi
 
MAGONJWA YA MFUMO WA CHAKULA:
 Kiungulia au Vidonda vya tumbo
 Michubuko au vijidudu kwenye njia ya chakula (oesophagitis)
 Magonjwa mengine ya njia ya chakula, tumbo, kongosho au hata ini.
 
Dalili:
 Husababisha maumivu ya kifua hasa sehemu ya chini, katikati ya matiti,
 Huweza kuwa kama moto, au maumivu tu makali katika eneo hilo
 Wakati mwingine husikika sehemu ya chini ya moyo upande wa kushoto
 
Usambaaji wake(radiation) huelekea upande wa bega la kulia au mgongoni
 Mara nyingi huwa na uhusiano na chakula – maumivu wakati wa kumeza, baada ya kula, wakati mtu ana njaa, baada ya kula aina fulani ya vyakula, au akibadilisha utaratibu wa chakula.
 Kama tatizo limeshakuwa kubwa huweza kusababisha maumivu makali hata bila kuhusiana na chakula.
 
MAGONJWA YA NGOZI, MISULI NA MUFUPA YA KIFUA
 Moto wa mungu (Herpes zoster) kwenye eneo la kifua
 Magonjwa ya matiti
 Magonjwa ya mifupa au vishikizo vya uti wa mgongo
 Magonjwa ya mishipa ya fahamu ya kufua
 Michubuko, kuumia au kuvutika kwa misuli katika kifua
 
Michubuko, vijidudu au kuumia mifupa, viungo(joints) au vishikizo vya viungo(tendons and ligaments) katika eneo la kifua
 Magonjwa mengine ya misuli na mifupa ya kifua
 
Dalili:
 Maumivu yanayosababishwa na magonjwa haya huweza kufana na maumivu yeyote yaliyotajwa hapo juu.
 Ni muhimu kujua historia au maelezo ya maumivu hayo kwa undani, kufanyiwa uchunguzi wa kina na vipimo pale vinapohitajika ili kujua tatizo.
 
MAGONJWA MENGINE NJE YA KIFUA YANAYOWEZA KUSABABISHA KIFUA KUUMA
 Magonjwa ya kisaikolojia au kuhema haraka karaka
 Sumu za aina fulani kama – lead, carbon monoxide
 Magonjwa ya Saratani
 
MUHIMU:
Magonjwa yanayosababisha maumivu ya kifua, hasa yatokanayo na moyo au mapafu huweza kusababisha kupoteza maisha haraka sana kama yasipotibiwa kwa wakati. Tafadhali wahi hospitali ili upatiwe tiba mapema na kuokoa maisha yako. Usipuuzie maumivu ya kifua; Ni afadhali kumsumbua daktari kwa kuwahi hospitali na kukuta hakuna tatizo, kuliko kuogopa kumsumbua daktari halafu ukachelewa hospitali na kupata madhara ambayo yangeweza kuzuilika, au kupoteza maisha.
 
5FACFA8B-EE6B-4DBC-91AC-F858DA1B3CEB.png
 
Back
Top Bottom