Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Kama ulikuwa hujagundua chai ya kijani kama nzuri, huu ni wakati muafaka wa kufanya hivyo! Chai Hii hunywewa sana nchi za Asia, pamoja na kwamba chai hii hunywewa kama chai nyingine za kwaida, bila kusahau chai hii ni zaidi ya chai kwani ni muhimu sana kiafya. Chai ya kijani tajiri katika antioxidants, na pia inasaidia sana, kuyayusha mafuta mabaya (Fat) na kupunguza uzito, pamoja ya Kufurahia kikombe cha chai moto na harufu nzuri ya chai ya kijani pia chai ya kijani hukuletea neema kubwa katika mwili wako.