Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Alisema mwamuzi hakutoa uamuzi sahihi katika baadhi ya matukio na kitendo cha kumtoa kwenda jukwaani ulikuwa uamuzi mkubwa zaidi.

Kocha huyo alilalamika kuwa Man City haikutendewa haki katika mchezo wa kwanza akidai bao la Mohamed Salah halikuwa halali kwa kuwa alikuwa ameotea.
 
Rais wa Barcelona Josep Bartomeu ameomba radhi mashabiki wa klabu hiyo baada ya timu hiyo kutupwa nje katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Barcelona iliyokuwa ikipewa nafasi ya kusonga mbele, iliondolewa na AS Roma ya Italia baada ya juzi usiku kuchapwa mabao 3-0 ugenini.
 
AS Roma imesonga mbele kwa faida ya bao la ugenini licha ya timu hizo kutoka sare ya jumla ya mabao 4-4.

Mbali na kutupwa nje, kibarua cha kocha Ernesto Valverde kinaweza kuoya nyasi kutokana na matokeo hayo ambayo hayakutarajiwa na mashabiki wa soka.
 
Kigogo huyo alisema amepokea kwa masikitiko matokeo hayo na hana njia nyingine zaidi ya kuwaomba radhi mashabiki wa klabu hiyo ya Noy Camp.

“Naomba radhi sana. Roma walikuwa katika kiwango bora uwanjani na walikuwa sahihi kusonga mbele. Vijana walipambana lakini hali imekuwa tofauti na matarajio,”alisema Rais huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…