Je! mlo uliokamilika ni upi?
Hili ni sawali ambalo watu wengi hujiuliza na hivyo ni vyema kufafanua swala hili. Mlo kamili ni ule amabo uliojumuisha ania tano ya vyakula ambavyo ni maziwa, matunda, nafaka, nayama zisizo na mafuta/karanga pamoja na mboga/kunde.
Maziwa ni moja wapo ya aina ya chakula ambacho kina umuhimu sana katika mwili wa mwanadamu hasa kutokana na virutubisho vilivyo ndni yake. Chakula hiki kimebarikiwa na kalisi (calcium) ambayo husaida kuhimarisha mifupa ya mwili.
Matunda ni aina ya chakula kilicho barikiwa kwa kuwa na vitamini ukilinganisha na aina nyingine ya vyakula hivyo na pia chakula hiki huwa na kambalishe. kwa kula matunda kunafanya ngozi ya mwili kuonekana yenye afya na mwili kuonekana imara.
Nafaka ni aina ya chakula kilichobarikiwa kwa kuwa na kamba-lishe na wanga ambapo huongeza nguvu na afya ndani ya mwili. Vyakula vilivyotokana na nafaka ni kama vile supageti na mkate.
Mboga na kunde ni aina moja wapo ya kundi la chakula ambacho huliwa sana na watu wengi katika maisha ya kwaida. Chakula hiki kimebarikiwa kwa kuwa na vitamini, kamba-lishe, pamoja na lishe ya mimea(phyto-nutrients)
Aina hizo za vyakula vikizingatiwa kwa kuliwa katika mlo wa kila siku mtu anaweza akuweka mwili wake katika muonekano mzuri na hata kwa wale wanaopenda kupungua ama kuongeza mwili wanaweza wakafanya hivyo kwa kukadiria kiasi cha kila aina ya chakula wanachokula.
Kwa mtu anayetaka kuongeza mwili atalazimika kula vyakula vya (Nafaka, Nyama/karanga, Maziwa) kwa sana ili apate kamba-lishe, protini na wanga kwa sana.
Kwa mtu anayetaka kuongeza mwili atalazimika kula vyakula vya (Nafaka, Nyama/karanga, Maziwa) kwa sana ili apate kamba-lishe, protini na wanga kwa sana.