Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Screenshot_2018-04-11-23-21-46.jpg
 
Siku zote katika maisha njisi unavyoonekana ni matokeo ya lishe yako ya kila siku.Tangu unapokula asubuhi mpaka jioni huamua afya ya mwili wako iweje.Hivyo basi hata katika swala zima la afya ya ngozi yako inategemea unakula nini.Kumbuka chakula unachokula kinaweza kikajenga afya yako na kuwa imara au kudhorota afya yako na kuwa dhaifu.
 
Afya ya ngozi yako ni sehemu moja muhimu sana kuipa umakini.Watu wengi huwa hawajui siri iliyopo katika vyakula tunavyokula katika kuboresha au kubomoa afya ya ngozi zetu.Baadhi ya watu huwa wanaangaika kutafuta mafuta ya kikemikali kuhakikisha ngozi zao zinakuwa vizuri pasipo kutambua kile wanachokula ndio kitaamua afya ya ngozi yako iwe katika hali gani. Leo nataka nikufumbue macho katika hili ili ufahamu umuhimu wa vyakula tunavyokula
 
Wataalamu wa afya wanasema kila kitu tunachokula ni sehemu ya miili yetu ikiwa ni pamoja na muonekano wa nje(ngozi).Hivyo kadiri utakavyoendelea kula chakula bora ndivyo afya ya ngozi yako itazidi kuimarika zaidi.
 
Back
Top Bottom