Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hata hivyo siku iliyofuata yaani Aprili 6 alirudi akiwa na panga mkononi na kuamua kuezua mabati ya nyumba zote mbili. “Nilimuarifu balozi na majirani wakaja, akakaidi tukatoa taarifa polisi hawakufika, ikabidi wataarifiwe makamanda wa mgambo na kufanikiwa kumkamata na kumpeleka kituo cha polisi na kuwekwa mahabusu.
 
Kiini cha Mgogoro

Anadai kuwa kiini cha ugomvi wao ni yeye Mariam kuzaa watoto wa kike, wa kwanza ana miaka 15 yuko kidato cha kwanza Mugumu Sekondari, wa pili ana miaka 12 yuko darasa la sita, watatu ana miaka 9 anasoma darasa la tatu na wa miaka 4 na nusu yuko chekechea wote wako Kambarage Shule ya msingi.
 
Anadai kuwa alilazimika kuoa mke mwingine na baada ya kupata mtoto wa kiume ndipo akazua vurugu za kuuza nyumba na kususia kuhudumia familia wakalazimika kufikishana mahakamani baada ya kushindikana kwenye ngazi nyingine za kitongoji na kuamriwa asiuze nyumba na aendelee kutoa matumizi kwa familia
 
Mwenyekiti

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chamoto, Rhobi Magoiga anasema mgogoro wa familia hiyo ulikuwa wa mara kwa mara na tatizo ni kuzaa watoto wa kike. “Tumejitahidi kusuluhisha mpaka tukawatuma mahakamani na kutolewa maamuzi ya kuwa hatakiwi kuuza nyumba kwa kuwa ni mali ya familia,” anasema.
 
Majirani

Mwita Zakayo ambaye ni jirani yake anasema kitendo hicho ni cha kikatili kwa kuwa kimeathiri hadi watoto, baada ya kuzuiwa usiku alishangaa kuona asubuhi amekuja na kufanya ukatili mkubwa zaidi ya ule wa jana yake.
 
Jirani mwingine Paulo Marwa anasema vitendo kama hivyo ni kama mauaji na vinazidi kuwachafua Wakurya katika maeneo mengine, “huyu hawezi kuingia ndani ya nyumba hii, tukio hili ni sawa na kuchoma vitu vya mke wako ama kuua, unawezaje kuezua nyumba na watoto wakiwa wamelala ndani, huu ni unyama, ” anabainisha.
 
Watakiwa kutambikiwa

Marwa anasema ili kumaliza mikosi mtuhumiwa anatakiwa kununua kondoo na vitu vingine ili wazee waweze kuwafanyia matambiko vinginevyo madhara yatakuwa makubwa kwa familia hiyo.
 
Kuna imani kuwa kama wakiingia ndani ya nyumba hiyo lazima familia zao zipate matatizo ikiwemo matukio yasiyokuwa ya kawaida, kwa misingi hiyo hapa lazima ijengwe nyumba nyingine kwa ajili ya huyu mama,” anasema.
 
Anasema kuwa lengo lake lilikuwa ni kumkomoa mke na watoto, kitendo cha yeye kupanga chumba huku mke akiwa ndani ya nyumba hiyo, hata hivyo analaani njia aliyotumia kwa kuwa ni laana kubwa kwake na jamii yake.
 
Naomba sheria ichukue hatua stahiki kudhibiti vitendo kama hivi maana huyu ni mkwe wangu nimejitahidi kusuluhisha bila muafaka, akaamua kuoa na bado ameendelea kumfanyia unyama huo,” anasema.
 
Kaka wa Isaya ataka apimwe akili

Richard Petro kaka wa mtuhumiwa anasema kuwa amechoshwa na vitendo vya mdogo wake kwa kuwa vinamtia hasara. “Amegombana na mkewe akaoa mke wake yuko kwangu sasa anaezua nyumba anategemea waishi kwa nani, nasema siwezi na hata Polisi sitaenda atahangaika na hali yake mwenyewe,” anasema.
 
Ameamuru vitu vyote alivyochukua kwa mke wake na kuvipeleka kwake virudishwe huku akimtaka akiachiwa atafute namna ya kumjengea mke wake nyumba. “Nadhani huyu anatakiwa kupimwa akili maana haiwezekani mwenye akili timamu akafanya mambo kama haya,” anasisitiza.
 
Watoto

Watoto wa Isaya Petro wakiongozwa na yule mkubwa wanaomba msaada kwa jamii kwa kuwa uamuzi wa baba yao kuwafanya kukosa makazi pia utawaathiri kimasomo kwa kuwa hawajui hatima yao.
 
Mtuhumiwa ajitetea

Isaya Petro akiwa chini ya ulinzi mbele ya familia yake na majirani anasema kuwa yeye aliamua kuezua nyumba ili akajenge kijijini kwa kuwa maisha ya mjini yamekuwa magumu. “Watoto wamekua nilitaka nihamie kijijini lakini mke wangu hataki ndiyo maana nikaezua.” anasema.
 
Anakiri kuwepo mgogoro wa muda mrefu hadi mahakamani lakini ulihusisha yeye kutohudumia familia, kuhusu suala la watoto wa kike anasema ni kweli mke wake amezaa watoto wanne wa kike. “Niliamua kuoa mke mwingine amezaa watoto wawili wa kike na wa kiume, hilo si tatizo,” anasisitiza.
 
Hata hivyo anakiri kuwa kwa muda mrefu amekuwa akiishi na mke mdogo baada ya kutokea mgogoro baina yao na hata hakumshirikisha kuhusu uamuzi huo wa kuhamia kijijini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…