Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Watetezi

Gabriel Simioni Mwenyekiti wa Shirika la Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu la Geitasamo anasema watashirikiana na huyo mama kuhakikisha haki yake inapatikana kwa kuwa moja ya mambo yanayoufanya mkoa wa Mara kuwa miongoni mwa vinara wa ukatili ni mfumo dume.
 
Mali kama hiyo si ya mume tu bali ya familia, lakini kutokana na mfumo dume wa baadhi ya jamii wanaona wanawake kama wajakazi hawana haki juu ya mali, lazima tusimame imara ili iwe fundisho kwa wengine wanaotumia mifumo kandamizi kuwanyima haki wanawake,” anasema.
 
RPC atoa msimamo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Jafari Mohamed anasema mtuhumiwa watamfikisha mahakamani kwa kuwa kitendo hicho ni kosa la jinai. “Moja ya kazi zetu ni kudhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia kama huyo alivyofanya, taratibu zikikamilika tutamfikisha mahakamani,” anasema.
 
Nilipozaa watoto wanne wa kike kwangu nilichukulia kama jambo la kawaida, sikutegemea kama ingekuwa chanzo cha kuvuruga ndoa yangu na kufikia hatua ya mume wangu kuezua paa la nyumba ili nimwachie mji auuze,” anasema Mariam Jackson (33).

Uamuzi wa kikatili uliomuacha Mariam mkazi wa Chamoto, Mugumu wilayani Serengeti mkoani Mara akihangaika na wanaye wanne, maana kwa mila na desturi za Kikurya hataweza kuingia humo tena. Hata akitokea mtu wa kuezeka upya nyumba hiyo yeye wala mume wake hawawezi kuingia, anayefanya hivyo huchukuliwa kama muuaji aliyekwenda kinyume na mila, ni lazima kwanza afanyiwe tambiko na wazee.
 
Akiwa katika hali ya kukata tamaa huku akibubujikwa machozi, Mariam anasema kinachomtesa ni kuzaa watoto wote wanne wa kike wakati mume wake akihitaji mtoto wa kiume jambo ambalo yeye hana uamuzi nalo na sasa amejikuta akiishi maisha ya kutangatanga huku kaka akishauri mdogo wake aliyefanya unyama huo apimwe akili kwani hata yeye amechoka na visa vyake.
 
IMG-20180413-WA0013.jpg
 
Back
Top Bottom