Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, January Makamba amesema jukumu la ujenzi wa taifa ni la kizazi cha sasa ambacho kina wajibu wa kusisitiza amani, demokrasia na utulivu katika nchi.

Makamba ameyasema hayo leo Aprili 13, wakati akitoa hotuba yake kama mgeni rasmi katika Kongamano la Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere linalofanyika katika Chuo Kikuu cha Mwalimu Nyerere Kigamboni (Zamani Kivukoni).
 
Kizazi cha Baba wa Taifa Mwl Nyerere kilikua na jukumu lake la wakati ule ambalo lilikuwa ni kukabiliana na changamoto ya kutawaliwa na walifanya wajibu wao hakuna tunachowadai tena, na sisi kizazi cha leo tuna misingi yetu ambayo ni kutatua changamoto za kitaifa zilizopo," amesema Makamba.
 
Mtandaoni ukiangalia leo vijana wanajikita zaidi kutafuta taarifa na si maarifa yenye tija kwa taifa leo, angalia leo katika mtandao wa YouTube utakuta video ya Seduce Me au Nampa papa ya Gigy Money ina views wengi kuliko hotuba ya Mwalimu Nyerere," amesema Makamba.
 
Wageni wengine waliohudhuria kongamano hilo ni Waziri Mkuu mstaafu Joseph Warioba, Spika wa Bunge Mstaafu Annie Makinda, Waziri mstaafu Profesa Mark Mwandosya, Mwenyekiti wa bodi ya Parole Augustino Mrema na viongozi wengine.
 
Licha ya kufungiwa maisha kujihusisha na masuala ya soka, aliyekuwa makamu wa rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura bado ana ndoto ya kurudi kuongoza shirikisho hilo kabla ya Juni.

Wambura kupitia wakili wake, Emmanuel Muga alidai jana kwamba siku si nyingi atarudi kuongoza TFF na Juni atashiriki kongamano la Fifa ambalo amealikwa kama makamu wa rais wa TFF.
 
Wambura atarejea kwenye nafasi yake siku si nyingi, hilo halina ubishi," alisema Muga na kufafanua kinachowapa imani hiyo.

"Tumejipanga kwenda CAS (Mahakama ya usuluhishi michezoni), huko tutapata haki yetu na Wambura atarejea kuongoza TFF, mechi ya nyumbani imekwisha sasa TFF itakwenda kucheza ugenini," alisema Wambura akimaanisha mechi ya ugenini ni kesi yao kusikilizwa CAS.
 
Wakili huyo alidai kinachowachelewesha kupeleka kesi yao CAS ni nakala ya hukumu ambayo wamekuwa wakizungushwa kuipata tangu rufaa yao ilipotangazwa kutupwa.

"Leo 'jana' Wambura amekwenda mara mbili TFF kufuatilia nakala ya hukumu na kuambiwa imefungiwa kabatini lakini hicho hakiwezi kuturudisha nyuma katika mapambano ya kudai haki.
 
Back
Top Bottom