Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mwezi Juni Wambura amealikwa kushiriki kongamano la FIFA, hivyo wamejipanga kuona mteja wangu anapata haki yake, anarejea kwenye wadhifa wake TFF na anashiriki kongamano hilo akiwa makamu wa rais TFF," alisema Muga.

Alisema mpango wa kupeleka kesi yao kwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe na kwenye Baraza la Michezo la Taifa (BMT) haupo tena.
 
Tutakakopatia haki yetu ni CAS pekee, huko ndiko tunaelekea japo tunazungushwa kupewa nakala ya hukumu lakini hiyo ni haki yetu watake wasitake watatupatia," alisema Muga.

Wambura alifungiwa na kamati ya maadili kwa makosa ya kupokea/kuchukuwa fedha zaTFF za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanuni za maadili za TFF Toleo la 2013
 
Jingine ni kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya Jekc System Limited huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za maadili za TFF Toleo la 2013

Kufanya vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa 2015.

Kigogo huyo aliyekumbana na misukosuko kwenye soka mara kadhaa alikata rufaa kwenye kamati ya rufaa ya maadili ambayo nayo ilitupiliwa mbali.
 
Klabu ya Atletico Madrid inatarajiwa kumuaga kwa heshima mshambuliaji nguli Fernando Torres.

Torres anatarajiwa kuihama klabu hiyo, baada ya kucheza kwa miaka 15 katika kikosi hicho. Ujio wa Diego Costa umemuondoa nyota huyo katika kikosi cha kwanza.
 
Atletico Madrid imepanga kumuaga mshambuliaji huyo katika mchezo dhidi ya Elbar kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano.

“Ana sifa za kuagwa kwa heshima kwasababu ni mchezaji ambaye hatutamsahau kwa huduma yake nzuri,”ilisema klabu hiyo.
 
Short-Hairstyle-Black-Women-1-396x300.jpg
 
Mchezo huo utakuwa wa mwisho kwa timu hizo msimu huu na Torres atapewa heshima baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio.

Mkataba wa Torres unatarajiwa kumalizika msimu ujao wa majira ya kiangazi na hii itakuwa mara ya pili kuondoka Atletico Madrid.
 
Mwaka 2007 alijiunga na Liverpool kabla ya kutimkia Chelsea na baadaye AC Milan mwaka 2016.

“Fernando ni mchezaji nguli katika klabu hii, siku zote amekuwa na mtazamo chanya kwa klabu yetu, tunamshukuru kwa huduma yake na hapa ni nyumbani kwake,”ilisema taarifa ya klabu.

Klabu hiyo ilisema milango ilikuwa wazi kwa Torres endapo angetaka kumalizia soka yake Atletico Madrid.
 
Mshambuliaji nguli wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic amedai ana uhakika wa kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), limemuwekea vikwazo nahodha huyo wa Sweden kucheza fainali hizo kwa kuwa ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya kucheza mchezo wa kubahatisha.
 
Hata hivyo, Ibrahimovic ameivimbia Fifa baada ya kudai kuwa ana matumaini ya kucheza fainali hizo kwa kuwa hilo ni suala binafsi.

“Fifa haiwezi kunikataza nisishiriki fainali za Kombe la Dunia Russia. Ni uamuzi binafsi, nitakwenda na nitakuwepo,”alisema mshambuliaji huyo mwenye miaka 36.
 
Fifa imemtaka nyota huyo wa zamani wa Manchestre United kuvunja mkataba na kampuni hiyo ili kupata kibali cha kucheza fainali hizo.

Nguli huyo anataka kupeleka makali katika fainali hizo baada ya kujiunga na Los Angeles Galaxy ya Marekani
 
Back
Top Bottom