Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

749D518B-FF36-469A-A2AB-09BDD6D10A91.jpeg
 
Sanduku la Agano lilikuwa ni zaidi ya nyuklia, yaani ukiwa nalo vitani lazima ushinde.
Ukisoma vizuri Biblia wanasema lile ndiyo kilikuwa kiti cha enzi cha Mungu hapa duniani, ndiyo maana wakakiita Mercy Seat (Kitu cha Rehema) na wakina Mussa waliambiwa watengeneze kiwe mfano wa kile cha Mbinguni. Ndiyo maana ukiangalia picha zake unaona Makerubi (The Covering Cherubim) wako juu yake. Ukiangalia picha zaidi za Mungu (YHWH) watu wa kale hasa waajemi walimchora amepanda malaika (Cherubim) mwenye taili moja chini kama ilikvyokuwa kwenye sanduku la agano.

Makuhani walivyokuwa wanaenda kwenye hema ya kukutania waliambiwa wajiandaee Wiki nzima kwa kufua mavazi yao,
Hakuna kulala na mwanamke wala kula vitu najisi. Halafu siku ya ibada anaingia mle ndani huku amejifunga kengere kiunoni na kamba ndefu mguuni ambayo imetoka hadi nje kwa wakuhani wengine. Akiwa anavukiza uvumba inabidi awe anapiga kengere ili kuonesha kama bado mzima na kama hapigi kengere wanajua keshakata basi wanavuta tu ile kamba ndefu iliyokuwa imefungwa mguuni mwake. (Teh teh teh teh teh)

Kwenye kitabu cha Mambo ya Nyakati wa Pili mfalme Uzziah Bwana alikuwa ni moja kati ya wafalme wa Israeli waliowahi kuwa na nguvu sana ukiwatoa Suleimani, Daudi na Ahabu. Alipigaa vita za hatari na baadhi ya wanahistoria wanasema kwa mara ya kwanza Silaha nzito za vita kama Catapult na Siege Engines nyingine zilianza kutumika na huyu mfalme hadi wengine wanasema yeye ndiye alizigundua. Falme za Jirani kama Ethiopia, Libya na Ashuru walikuwa wanamwogopa sana maana alikuwa hajawahi kushindwa vita tangia kawa mfalme na miaka 16.

Sasa kuna siku akajisahau akasema lazima na yeye aende mahali Patakatifu kwa watakatifu lilipo sanduku la agano ili akamvukizie Mungu uvumba. Makuhani walimkataza sana asifanye hivyo kwasababu ni wana a MUSSA, Haruni na Walawi walikuwa wanaruhusiwa kuingia mle. Jamaa akaingia kwa nguvu Mungu akachukia akamtandika Ukoma usoni mwake. Makuhani walisikitika sana na ikabidi wakamfungie kwenye chumba chake peke yake miaka yake yote hadi anakufa.

NB: Mfalme Daudi peke yake ndiye aliyewahi kuvunja hizi protokali, na hakufanywa lolote na Mungu kwasababu wanahistoria wa Theolojia wanasema alikuwa anapendwa sana sanaaa na Mungu. Kuna mikate ya wonyesho ilikuwa hairuhusiwi kuguswa na mtu na inakaa madhabahuni na imekaa kama urembo na ukishika tu unakata pale pale. Jamaa lilikuwa linaumwa njaa likaingia pale likafyala yote na likawapa wasaidizi wake na Makuhani wakaona jamaa limetoka zima na halifi kabisa wakajua basi huyu kuna Mkataba binafsi waliofanya na Mungu...

Wafilisti waliliiba kipindi cha Sauli anakufa na wakalipeleka kwao ili Waisraeli wasishinde vita tena.
Eeh bwana nchi nzima ilipigwa majipu hadi wale wachawi sugu wakasema jamani kama mnaweza mlirudishe tu.
Wagiriki (Seleucid) nao waliisoma namba baada ya kuchinjia kitimoto mbele ya hekalu na kuamua kuingiza Sanamu la Zeus hekaluni kwenye Sanduku la Agano...(mkuu ntaanzishia mada kabisa kuhusu hili nashukuru kwa kunikumbusha)
Somo zuri sana ndio maana wachina wakisoma Bible wanaona kama hadithi Fulani hivi lakini ndio ukweli
 
Back
Top Bottom