Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati Liverpool waliitoa Manchester City kwa jumla ya mabao 5-1, Roma walifanya maajabu kwa kuwatoa Barcelona kwa bao la ugeini baada ya kuchapwa mabao 4-1 katika pambano la kwanza Nou Camp kabla ya kushinda 3-0 katika pambano la marudiano jijini Rome.
 
Kwa kupangwa na Roma, staa wa Liverpool, Mohamed Salah anarudi katika uwanja wake wa zamani wa Olimpiki ambapo pia alitamba kabla ya kuuzwa kwa Pauni 34 milioni kwenda Liverpool katika dirisha kubwa liliopita la majira ya joto mwaka jana.
 
Kwa upande wa pambano jingine, Bayern Munich wataanzia nyumbani dhidi ya Real Madrid ikiwa ni mara ya saba katika misimu tisa wababe hao wa Ujerumani wakitinga katika hatua hiyo. Hata hivyo watakuwa wakiisaka fainali yao ya kwanza katika michuano hiyo tangu walipotinga mwaka 2013 Wembley na kuwadunda majirani zao Borussia Dortmund.
 
Bayern wametingia katika nusu fainali hizi baada ya kuichapa Sevilla mabao 2-1 shukrani kwa ushindi wao katika mechi ya kwanza waliposhinda 2-1 ugenini kabla ya kutoka suluhu katika uwanja wao wa nyumbani Allianz Arena.
 
Madrid ambao wamechukua mara mbili mfululizo, walitinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Juventus katika pambano lilojaa utata mwingi Jumatano usiku. Walishinda mabao 3-0 ugenini kabla ya kuchapwa 3-1 nyumbani Santiago Bernabeu shukrani kwa bao la kufutia machozi la Cristiano Ronaldo katika dakika ya mwisho lililowapa tiketi ya kutinga hatua hiyo.
 
Madrid wanapambana kuchukua taji hili kwa mara ya tatu mfululizo na endapo watafanikiwa kufanya hivyo watakuwa klabu ya pili kutwaa ubingwa huo mara ya tatu mfululizo tangu Bayern Munich ilipofanya hivyo mwaka 1976.
 
Wanariadha Caster Semenya wa Afrika Kusini na Mganda Joshua Cheptegei wameendelea kuwa mwiba mchungu kwa Wakenya katika makala ya 21 ya mbio za Jumuiya ya Madola, yanayoendelea kutimua vumbi Jijini Gold Coast, Australia.
 
Semenya aliendeleza ubabe dhidi ya Wakenya katika mbio za mita 800 alipompiku Mkenya Margaret Nyairera kuishindia Afrika Kusini medali ya 13 ya dhahabu, akitumia dakika 1:56.68 na kuweka rekodi mpya kwenye mashindano hayo.

Nyairera alimaliza wa pili, akitumia dakika 1:58.07. Wakenya wengine katika mbio hizo, Emily Tuwei na Eglay Nalyanya walimaliza katioa nafasi ya saba na nane mtawalia.
 
Saa chache baada ya Kenya kushindwa katika mbio mita 800, Mganda Joshua Cheptegei alishindilia msumari mwingine wa moto katika kidonda cha Kenya, kwa kushinda mbio za mita 10,000 baada ya kuwaburuza katika mbio za mita 5000 siku mbili zilizopita.
 
Cheptegei alitumia muda wa dakika 27:19.62 kuweka rekodi Mpya ya mashindano huku nafasi ya pili ikienda kwa Mohammed Ahmed wa Canada. Mkenya Rodgers Kwemoi wa Kenya, ambaye ni bingwa wa dunia kwa vijana, alimaliza wa tatu akitumia 27:28.66.

Wakenya wengine katika mbio hizo Jonathan Ndiku na Josephat Koech walimaliza katika nafasi ya nane na 10 mtawalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…