Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kamati ya Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, (TLS) iliyoundwa kujadili uamuzi wa Mwanasheria wa Mkuu wa Serikali (AG)wa kuzifanyia mabadiliko kanuni za uchaguzi wa chama hicho imesema, AG hakuwa na mamlaka ya kufanya mabadiliko yoyote.

Hayo yameibuka leo Aprili 14 wakati wa uchaguzi wa kumpata Rais mpya wa chama hicho, mjini Arusha.
 
Katika tukio hilo, Makamu wa Rais wa sasa wa TLS, Godwin Ngwilimi, ametoa hoja hiyo na kumtaka mjumbe wa Baraza la uongozi, Jeremiah Mtobesya kusoma mapendekezo hayo ambayo yalisema Mwanasheria Mkuu wa serikali hakuwa na Mamlaka ya kufanya mabadiliko bali kuyachapisha kwenye gazeti la serikali.

Pia walipendekeza kufuata njia za kiutawala kuonana na Mwanasheria Mkuu au kwenda mahakamani kutafuta tafsiri ya mamlaka yake kwa TLS.
 
Mgombea Urais wa TLS, Fatma Karume amesema maboresho yaliyofanywa hayana msingi wa kisheria kwa kuwa kanuni za uchaguzi wa TLS zinaanza kufanya kazi mara tu baada ya kupitishwa na mkutano mkuu.

Hata hivyo wajumbe hao walikubaliana na baraza la uongozi kutengeneza kanuni ambazo zitatamka kuwa si lazima zitangazwe kwenye gazeti la serikali ili ziwe halali.
 
Mtoto wa Winnie Mandela, Zenani Mandela, ametoa ‘dongo’ mbele ya waombolezaji wakati wa mazishi ya mama yake leo, katika Uwanja wa Orlando, Afrika Kusini.

Zenani amesema, mama yake aliporwa haki yake wakati wa maisha yake.

Leo maelfu ya watu wamekusanyika katika uwanja huo kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho mbele ya mwanamapinduzi huyo wa Afrika Kusini, ambaye pia aliwahi kuwa mke wa Nelson Mandela.
 
Zenani alivicharukia vyombo vya habari na kusema kuwa vilitumika kumchafua mama yake.

“Kwa nini waliukalia ukweli na kusubiri hadi mama yangu afe ndiyo wauseme. Wamepora urithi wa haki wa mama yangu wakati wa uhai wake,” amesema Zenani huku dada yake Zindzi akiwa pembeni yake.

Alionyesha kukasirishwa na kauli ya Kamishna wa zamani wa Polisi nchini humo, George Fivaz, ambaye wiki iliyopita baada tu ya kifo cha Winnie, amesema, hakuna kinachomuhusisha Madikizela Mandela na kifo cha Stompie Seipei.
 
Inadaiwa kuwa Winnie alihusika na kifo cha Stompie Seipei kijana wa miaka 14, mwaka 1989.

Zenani amesema, wale wote waliomfanyia mabaya mama yake, wasifikiri hata mara moja familia itayasahau mabaya hayo.

“Kumsifia sasa hivi, kunaonyesha wazi jinsi ulivyo mnafiki,” amesema Zenani akimtaja Fivaz.

Ameongeza: “Maumivu aliyoyapata maishani mwake, yapo kwetu.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…