Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

445217014_305072.jpg
 
Mwembe hustawi katika maeneo ya joto na nyanda za chini. Mti unafikia urefu wa meta 25, huota maeneo yote ya tropiki. Jina la kibotania huitwa mangifera indica, na waingereza huita mango, wandali na wanyakyusa huita umwembe. Maembe hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Tabora, Pwani, Mtwara, Tanga, Mwanza, Morogoro na Mbeya. Maembe ni zao muhimu la biashara na chakula.
 
Sehemu zinazotumika ni, Majani Machanga, matunda, kokwa (mbegu), magome (gamba), maua, mizizi nk. Ili kuyalinda maisha ya mti, chukua magamba kutoka kwenye matawi tu (na iwe kutoka upande mmoja tu)
Tunda hili, licha ya ladha yake nzuri pamoja na utamu wake, linaweza kutumika kwenye milo yote kwa siku kwenye familia nzima.
 
Ulaji wa mara kwa mara wa tunda hilo husaidia kupunguza kiwango cha asidi mwilini, kuboresha mmeng’enyo wa chakula na kurekebisha kiwango cha insulini. Husaidia kusafisha damu pia, kuimarisha muonekano wa ngozi, kuzuia saratani na kuimarisha kinga ya mwili. Hupunguza mawe kwenye figo. Faida nyingine ni kuongeza madini ya chuma kwa wajawazito, kupunguza uzito na kulinda macho dhidi ya magonjwa.
 
Vilevile juisi hii inasifika kwa kuimarisha mmeng’enyo wa chakula na huondoa ukosefu wa choo ikichanganywa na nanasi.
Licha ya vitamin A, juisi ya embe ina vitamin C pamoja na carotenoids ambazo husaidia kurekebisha kinga za mwili hivyo kuwafaa zaidi wenye upungufu wa kinga hizo, wanaonyemelewa na magonjwa au wenye maradhi ya muda mrefu mfano pumu.
 
Back
Top Bottom