Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic anasema ananafasi kubwa ya kuchezea timu ya Sweden katika michezo ya kombe la dunia nchini Urusi,licha ya kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amestaafu kucheza soka ya kimataifa tangu 2016 (Sun)
 
Mkuu wa Newcastle Rafael Benitez anatarajia kufanya mazungumzo na mmiliki wa timu, Mike Ashley kabla ya kusaini mkataba mpya . Benitez anataka kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha za kufanyia usajili wa wachezaji katika msimu wa majira ya joto kabla ya kuingia katika klabu hio.(Telegraph)
 
Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United na Tottenham wanampango wa kurejea juhudi za kupata fedha zaidi kutoka kwa marupurupu wanaolipia nchi za nje kutangaza mechi za Premier League. (Mail)
 
Mwanamuziki Koffi Olomide ametangaza kuwa na onyesho la muziki mwezi huu tarehe 24 nchini Kenya.
Onyesho hili litakuwa la kwanza nchini Kenya tangu alivyokataliwa kuingia nchini humo Julai 2016 baada ya kumdhalilisha mmoja wa wanenguaji wake .
Koffi amesema hayo katika ujumbe wa video kwamba amealikwa kufanya onyesho katika mkutano wa taifa la Kenya ambao utajumuisha viongozi 47 wa nchi hiyo ambao ni mjumuisho wa rais na viongozi wa juu wa serikali.
 
Mwanamuziki huyo Koffi Olomide anayefanya muziki wa lingala mwenye umri wa miaka 61, aliomba radhi mara kadhaa kutokana na utovu wa nidhamu aliouonyesha nchini Kenya kwa kumpiga mnenguaji wake.
Katika tangazo la video lilowekwa kwenye mtandao wa Youtube inayotambulisha ziara yake mpya ya muziki,Koffi ameonekana akiwaambia mashabiki wake wa Kenya kuwa anawapenda sana na anawakumbuka sana
 
Tukio lililomtia utatani lilirekodiwa katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta ambako alikuwa amewasili kwa tamasha lilopangwa kufanyika nchini Kenya.
Wengi wa Wakenya walimkashifu vikali kitendo hicho huku maoni katika mitandao ya kijamii, kutpita mada ya [HASHTAG]#KickKoffiOlomideBackToCongo[/HASHTAG] kwenye Twitter walipendekeza afurushwe kutoka Kenya.
Olomide aliwahi kujitetea kwa kusema kuwa alikuwa akijaribu kumtetea mwanamke huyo kwani mmoja wa maafisa wa kike katika uwanja huo wa ndege alikuwa akiwasumbua wasichana hao wachezaji ngoma aliokuwa wakiandamana naye.
 
Utafiti umevumbua kwa nini baadhi ya maradhi ya saratani ni hatari kuliko aina nyingine ya saratani ingawa zinaonekana kufanana
Taasisi ya wanasayansi ya Francis Crick ilianzisha uchambuzi wa historia ya saratani kwa ajili ya kutabiri mustakabali wake
Utafiti kwa wagonjwa wa saratani ya figo unaonyesha kuwa baadhi ya uvimbe ''ni hatari'' huku nyingine zikiwa hazina madhara na wakati mwingine hazihitaji matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…