Katika mwaka wa 2008 makamishna wa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (ECK) wakiongozwa na marehemu Samuel Kivuitu, waliondolewa wakati bunge lilipounda Tume Huru ya Muda ya Uchaguzi (IIEC) kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi wa 2007.
Issack Hassan, aliyeongoza IIEC (baadaye IEBC), aliondolewa pamoja na wenzake mwaka 2016, walipoandamwa na madai ya ufisadi.