Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

hapa ni kwamba tusithubutu kufanya majumuisho kwa kuwaweka watu katika makundi fulani ya jumla jumla ya kinadharia. Kwa mfano kusema kuwa wanawake wote wanatabia fulani, ama wanaume wote wanatabia fulani ni makosa ya kiufundi.
 
Screenshot_2018-04-16-12-27-03.jpg
 
Sababu si kila mwanamke ana haiba inayofanana na mwanamke mwingine. Na pia haiba ya mwanamke huweza kubadilishwa kutokana na haiba ya mume aliyenaye. Yaani kama mwanamke huyo angeolewa na mwanamme mwenye haiba nyingine, mwanamke huyo huyo angekuwa na haiba nyingine kabisa.
 
Tabia ya mwanamke wa ndoa fulani inatokana na jinsi haiba yake iliyoingiliana na ile ya mume wake. Mke huyo japo anaonekana kuwa na haiba isiyoridhisha katika ndoa B angeweza kuwa na haiba njema zaidi laiti kama angekuwa na ndoa C na mume mwingine kabisa.
 
Back
Top Bottom