Madame kuna kitu sisi wanawake huwa sometimes tunajitoa ufahamu, tunafanya starehe zetu lakini pale mimba zinapotunga tunajitia kutokuwa tayari..Kama mtu haupo tayari kwanini usijikinge??
Ndo pale tunapoanza michezo ya ajabu ajabu ya kujaribu kuua viumbe visivyo na hatia..
Hii ndo huwa sababu kubwa sana ya kutoshika tena mimba/ mimba zinakuwa zaporomoka tu..
Simaanishi kuwa wote wanaokumbwa na tatizo hilo wanakuwa kwenye hatia hiyo la hasha!
Kuna matatizo mengine yanaweza kuwa ya mtu binafsi ( kiafya) hivo yote yanawezekana.
Ukweli anaujua yeye, kama kweli huwa zaporomoka au labda alishaharibu hivyo kushindwa kabisa kutunga..
Yote kwa yote naimani kuna kutubu na kusamehewa, kama alifanya hiyo michezo naimani atakuwa amejuta vya kutosha na ametubu vya kutosha..Na kama pia ni matatizo ya kiafya Mungu akamponye naye siku moja akaitwe MAMA..