Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Wakati kiungo Santi Cazorla akiwa na matumaini ya kurejea uwanjani muda mfupi ujao, Arsenal imeingia hofu kuhusu kumpa mkataba mpya.

Kiungo huyo fundi wa mpira wa Kihispaniola, yuko nje ya uwanja tangu Oktoba 2016 baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu mara tisa, lakini Cazorla ameibuka na kudai anataka mkataba mpya.

Mkataba wa Cazorla na Arsenal ya Profesa Arsene Wenger unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, lakini mwenyewe anataka kumaliza soka lake klabuni hapo.
 
WALIMUONA wa nini pale Stamford Bridge, lakini Borussia Dortmund wakasema mleteni huku tuwaonyeshe na sasa wameelewa.

Lakini Chelsea imesisitiza, kamwe haitamwacha straika wao Michy Batshuayi kwa pesa ya mboga na watakuwa tayari kukaribisha mazungumzo kama itawekwa mezani Pauni 50 milioni.
 
Batshuayi yuko kwa mkopo pale Dortmund, lakini baada ya kukoshwa na kiwango chake sasa wanamtaka jumla, lakini Chelsea inataka dau hilo kwanza ndipo iweze kumuachia.

Straika huyo wa Ubelgiji, amekuwa kwenye kiwango bora zaidi baada ya kutua Bortmund, ambapo awali alionekana kuwa mzigo kwenye kikosi cha Mtaliano Antonio Conte.
 
MATAJIRI wa Jiji la Paris, Paris Saint Germain (PSG) imeanza mchakato wa kusaka saini ya kiungo ghali wa Manchester United, Paul Pogba, ambaye kwa sasa anapitia kipindi kigumu chini ya Jose Mourinho pale Old Trafford.

Kipindi cha hivi karibuni uhusiano wa Pogba na Mourinho umeyumba kutokana na supastaa huyo wa Kifaransa kudaiwa kucheza chini ya kiwango na sasa huenda akawekwa sokoni.
 
Kwenye mechi ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya West Bromwich Albion, Pogba alitolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Martial, ambaye naye yuko njiapanda klabuni hapo kutokana na kugomea kusaini mkataba mpya.
 
Back
Top Bottom