Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Khamis amesema, ndugu yake huyo alianza kuugua tangu Januari mwaka huu na alianza kwanza matibabu mkoani Iringa, hali ilivyokuwa mbaya alimchukua kwenda kumuuguza Dodoma.

Amesema, ugonjwa mkubwa uliokuwa ukimsumbua ni kupungukiwa damu na kuvimba bandama na ndio anaamini umechukua maisha yake.
 
Kwa mujibu wa mdogo wake huyo amesema, shughuli za mazishi zitafanyika nyumbani kwa babu yake Area C mjini Dodoma na maziko yatakuwa saa kumi jioni.

Kwa upande wa msanii Afande Sele, amesema amesikitishwa na msiba huo kwani mwezi mmoja uliopita Jebby alimpigia simu na kumueleza nia yake ya kutaka wafanye video ya wimbo wa Swahiba.
 
Yaani ni mwezi tu umepita Jebby alinipigia simu na kuniambia anataka tufanye video ya wimbo wa swahiba, kwa kuwa ameona wasanii wengi wanazifanyia video nyimbo zao za zamani, nasikitika hatujalitekeleza hilo, leo napata taarifa kuwa amefariki,”amesema Afande Sele.
 
Wataalamu wa afya wamebaini kuwa wanawake huathiriwa zaidi na magonjwa ya akili ya kundi la sonona na kihoro kwa kuwa huumizwa zaidi na maisha ya ndoa na masuala ya uhusiano ukilinganisha na wanaume.
 
Sonona ni aina ya ugonjwa wa akili unaotokana na kusononeka na kukata tamaa.

“Lakini kwa upande wa wanaume, wao hupata magonjwa ya akili kutokana na uraibu (addiction) ya dawa za kulevya, bangi au pombe,” alisema Dk Kuganda
 
Alisema 2016 walifanya tafiti katika Wilaya ya Temeke kwa wasichana wajawazito wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 19 na kuangalia magonjwa ya kihoro (anxiety) na sonona ambayo ni makundi ya magonjwa ya akili na kubaini kuwa asilimia 20 kati yao walikuwa na sonona na kihoro.
 
Kwa upande wake, mtaalamu wa afya, Dk Christopher Peterson alisema aliwahi kufanya utafiti na kubaini kuwa mwanamke mmoja kati ya watano ana maradhi ya akili aina ya sonona, huku mwanaume mmoja kati ya 10 ndiye huugua sonona maishani
 
Mtaalamu wa masuala ya afya ya akili, Profesa John Adams wa Chuo Kikuu cha Oxford, Uingereza anasema wanawake ndiyo wanaosumbuliwa zaidi na maradhi ya sonona.

Anasema utafiti uliochapishwa katika jarida la Monitoring Psychology ambao alishiriki ulionyesha kuwa wanawake wanakabiliwa na matatizo ya akili kwa asilimia 40 zaidi ya wanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…