Wakati mechi ikionekana kama itamalizika kwa sare hiyo ya 1-1, Arsenal ilitumia vyema dakika nane za mwisho kufunga mabao matatu, yaliwekwa wavuni na Aaron Ramsey katika dakika 82 na Lacazette kufunga mara mbili katika dakika 85 na 89.
Mechi hiyo ilikuwa kama send-off kwa kocha Wenger, ambaye hatakuwa na kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa karibu miaka 22.
Mechi hiyo ilikuwa kama send-off kwa kocha Wenger, ambaye hatakuwa na kikosi hicho kwa msimu ujao baada ya kudumu kwenye timu hiyo kwa karibu miaka 22.
Wenger alitangaza kung’atuka wiki iliyopita, lakini taarifa za ndani zinafichua kwamba Mfaransa huyo ametimuliwa baada ya kudaiwa kwamba atalipwa fidia ya Pauni 11 milioni kufidia mwaka mmoja uliobaki kwenye mkataba wake
Imetoka sare mara sita na kuchapwa kwenye mechi 11 na kujikuta wakishika nafasi ya sita kwenye msimamo, pointi 11 pungufu ya kuifikia Tottenham Hotspur inayoshika nafasi ya nne, ambayo inatoa tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Mchezo mwingine wa ligi hiyo uliofanyika jana, Stoke City walishindwa kutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Britannia baada ya kubanwa na Burnley na kutoka sare ya 1-1.
Stoke walihitaji pointi tatu za kuwatoa kwenye hatari ya kushuka daraja, walianza vizuri na kutangulia kwa bao la Badou Ndiaye, lakini Burnley walikuja kuchomoa kupitia kwa Ashley Barnes na kuwaweka pagumu.
Baada ya staa huyo kupasia mipira nyavuni mara 41 kwenye mechi zote alizocheza msimu huu akiwa na Liverpool, Klopp alikumbana na swali anadhani mchezaji huyo anafaa kuuzwa kwa thamani gani kwa sasa.
Hapo ndipo walipomchokoza Mjerumani huyo ambaye aliamua kulichunia swali hilo linalomhusu mshambuliaji wake ambaye kwa msimu huu amefunga mabao 31 Ligi Kuu England na kufikia rekodi za wakali kadhaa akiwamo Luis Suarez, Cristiano Ronaldo na Alan Shearer kwa kufikisha idadi hiyo ya mabao kwa msimu mmoja wa ligi.
Hilo swali lenu halinivutii,” alisema Klopp, ambaye anafahamu wazi kabisa kiwango cha mchezaji wake anachokionyesha msimu huu kinavivutia vigogo kibao ambavyo huenda vikajaribu kwenda Anfield mwishoni mwa msimu kutaka kumsajili.