Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Ati nini? Ndo njia ya kugundua mafekero ya watu hiyo ama?
 
MAWAZO ya wengi yaliamini kwamba staa wa Liverpool, Mohamed Salah angekuwa mwanasoka bora wa England msimu huu. Na kweli amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa England msimu huu, lakini mtu mmoja amegoma.
 
Pep Guardiola, kocha wa Manchester City amesisitiza kwamba staa wa timu yake, Kevin De Bruyne alipaswa kuchaguliwa kuwa mwanasoka bora wa England msimu huu, tena kwa urahisi tu badala ya Mohamed Salah.
 
Staa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alifunga bao lake la 12 la msimu kwa shuti kali katika pambano dhidi ya Swansea juzi muda mchache kabla ya Salah kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa msimu, lakini Gurdiola anaamini kwamba pamoja na Salah kufunga mabao mengi msimu huu lakini De Bruyne ni bora zaidi.
 
Najua maoni yangu kuhusu tuzo hizi. Kwa mtazamo wangu, unapochambua miezi 10 iliyopita hakuna mchezaji aliye bora zaidi ya De Bruyne kwa maana ya mwendelezo wa ubora. Labda kwa namba (idadi ya mabao) kuna wachezaji wengi bora zaidi yake lakini hakuna mchezaji bora zaidi yake msimu huu. Kwangu mimi alikuwa bora sana.” alisema Guardiola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…