Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Hatimaye dege kubwa la kampuni ya Emirates lililotua jana jijini Dar es Salaam kwa dharura, limeondoka kuendelea na safari yake ya Mauritius majira ya saa 2:15 asubuhi, huku Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ikitaja siri ya dege hilo kutua Dar es Salaam.

Akizungumza kwa njia ya simu asubuhi hii, Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema rubani wa ndege hiyo kubwa duniani alikuwa na viwanja saba mbadala vya kutua baada ya dharura kutokea, lakini uwanja pekee uliomvutia ni wa Dar es Salaam.
 
Angeweza kwenda Johannesburg (Afrika Kusini) au Windhoek (Namibia), au Madagascar pale pua na mdomo, au angeenda Nairobi, au Maputo, lakini akaona atue Dar es Salaam," amesema Johari.

Ameeleza: "Wanachoangalia ni usalama wa nchi katika anga. Je, anaweza kutua vizuri? Je, ndege itatunzwa vizuri? Usalama ukoje?"
 
IMG_20180425_151153_146.jpg
 
Mtangazaji wa kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Casto Dickson, anatarajia kufunga ndoa na video queen, Anna Kimario 'Tunda' kabla ya mwaka kwisha.

Akizungumza na MCL Digital, Dickson amesema atafanya hivyo kwa kuwa ndio mwanamke anayeona anafaa kuwa mke.
 
Unajua nimekuwa na mahusiano na wanawake wengi, lakini kwa Tunda nimekuta vitu tofauti sana, kwangu namuona anafaa kuwa mke wa mtu tofauti na watu wa nje mnavyomuona na nitamuoa kabla huu mwaka haujaisha," amesema mtangazaji huyo.
 
Amesema watu wamekuwa wakihoji iweje niwe na mwanamke ambaye ameshawahi kuwa na mahusiano na wanaume wengine, nawaambia wanamuona hivyo kwa kuwa ni maarufu lakini ukweli ni kwamba kuna watu wa kawaida wameshawahi kuwa na idadi ya wanaume wengi kuliko hata Tunda.
 
Back
Top Bottom