Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

314DDE0B-B59A-4ECD-9493-20ADDA7BADD4.jpeg
 
Wengi wamejikuta wakiingia katika ugomvi na baadhi marafiki zao kutokana na kushirikiana katika uendeshaji wa biashara zao, bila kujali ukubwa wa mtaji walionao au uwekezaji waliofanya kwenye mradi husika.

Mara nyingi watu huamua kushirikiana ili kufanya biashara kutokana na ukaribu walionao na kuaminiana.
 
Watu hao wanaamua kushirikiana kwa lengo la kugawana mtaji kisha baada ya kipindi fulani waje wagawane faida.

Wapo waliojikuta wakiingia katika changamoto iliyosababisha kuua urafiki wao, kusambaratisha ndoto zao za kuwa wafanyabiashara wakubwa japokuwa walianza na mitaji midogo.
 
Pia, wapo marafiki waliounganisha nguvu pamoja na kufanya biashara kwa mafanikio makubwa kiasi cha kuwa mfano wa kuigwa katika jamii wanazoishi licha ya kukutana na changamoto katika biashara, lakini bado waliweza kusimama imara na kushinda vikwazo.
 
Hata hivyo, kuna mambo ya msingi unayopaswa kuyazingatia kabla hujaingia katika ushirikiano wa kibiashara ambayo ni pamoja na umuhimu kuchukua muda wa kutosha kujiridhisha kama kweli unayetaka kushirikiana naye anaweza kuheshimu na kutekeleza majukumu mliyojipangia katika kuanzisha biashara, ili hatimaye muweze kukuza mtaji.
 
Jambo lingine ni awe mwenye kuridhika na kile anachopata badala ya kuwa na tamaa ya kupata sehemu kubwa ya faida inayopatikana, hasa kwa kutumia hila na udanganyifu kama vile kudai aliuza bidhaa kwa bei ya chini wakati uhalisia aliuza kwa bei kubwa na ya juu iliyozalisha faida ya kutosha.
 
Mnapoanzisha biashara ni lazima kujua aina ya bidhaa mnayotaka kushughulika nayo mfano kusafirisha bidhaa ndani na nje, kuuza dukani na kuuza kwa jumla kwa watu wenye maduka ya rejareja.
 
Vilevile, ni vyema kuangalia nani amewekeza mtaji mkubwa na mpange njia bora ya kugawana faida kwa kuwa mgawanyo wa faida imekuwa mojawapo ya changamoto kwa baadhi ya marafiki waliokubaliana kuanzisha biashara ya pamoja hasa kama mtaji uliotumika mwanzo kuanzisha haulingani.
 
Back
Top Bottom