Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo anawachanganya sana mabeki.
Inawezekana jana mechi ya Bayern Munich na Real Madrid walimwekea ulinzi wa nguvu asifunge, kumbe walikuwepo Marcelo na Marco Asensio, wenyewe walikuwa wakiangalia picha lote.
Bayern wakiwa nyumbani Allianz Arena, walijua kuwa wakikata umeme kwa Ronaldo, mambo yatakuwa yamemalizika wakaibuka Marcelo na Asensio wakamaliza mchezo, Bayern wakashangazwa kwa kupigwa mabao 2-1. Bao lao lilifungwa na Joshua Kimmich mapema kabisa.