Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FOMU nzuri ya straika wa Lazio, Ciro Immobile msimu huu imewaacha wadau wengi wa soka la Italia hoi huku baadhi yao wakiamua kumsifia mke wake Jessica Melana kwa mabadiliko hayo.

Msimu huu Immobile amekuwa kwenye fomu ya kutisha akifunga magoli 41 kwenye jumla ya mechi 45 alizopangwa hadi kufikia sasa.
 
Mara ya mwisho aliyokuwa katika ubora huu ni zamani kidogo kipindi akiwa anaichezea Torino na alifanikiwa kufunga magoli maradufu kama msimu huu.

Baadaye alihamia Borussia Dortmund alikochemsha kweli kweli akishindwa kutamba. Mambo yalipokuwa magumu aliondoka huko Ujerumani na kutimkia zake Uhispania kukipiga katika klabu ya Sevilla na huko tena akawa ovyo kabla ya kuamua kurudi Italia, mwanzoni mwa msimu huu akijiunga na Lazio.
 
Tangu arejee nyumbani Italia, Immobile amekuwa moto wa kuotea mbali na takwimu za msimu huu zikitosha kueleza.

Kwa fomu hii, ni mmoja wa wachezaji ambao alipaswa kuwa kwenye Kombe la Dunia kupambania kiatu cha dhahabu lakini kwa bahati mbaya hatakuwepo.
 
Liverpool ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Anfield ilishinda mabao 5-2 katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi usiku.

Tukio hilo lilitokea nje ya klabu ya usiku ya Albert na shabiki huyo aliwahishwa hospitali kwa kutumia gari la wagonjwa baada ya kuumia vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…