Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Thamani ya binadamu haiishii kwenye kifo. Hii ndiyo sababu binadamu akifa, ndugu, jamaa, marafiki na wote waliomfahamu huendelea kuupa thamani mwili wa marehemu kabla na baada ya kuhifadhiwa kaburini.

Hata heshima kwa mwili uliokufa haikomi baada ya maziko bali huendelea kwa namna nyingi, kama kuuombea dua, kujengea kaburi na kulifanyia usafi kila baada ya muda fulani.
 
Ndio maana kila jamii au dini zimejiweka utamaduni na taratibu za kidini za kuzika, ikiwa ni njia ya kuonyesha heshima kwa wapendwa wao waliopoteza maisha.

Mfano kusoma wasifu wa marehemu mbele ya kusanyiko, kutoa heshima za mwisho, kaburi kuwekwa mashada ya maua, na hata kuweka picha ya marehemu katika kuonyesha thamani ya mtu aliyewatoka.
 
Screenshot_2018-04-29-18-54-58.jpg
 
Lakini hayo hayakufanyika kwa zaidi ya miili 1,000 iliyokosa ndugu wala jamaa wa karibu wa kuwaandalia taratibu hizo na kuonyesha heshima kwa mambo waliyofanya wakati wakiwa hai.

Uchunguzi uliofanywa na Mwananchi unaonyesha kuwa maiti 1,206 zilizikwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia Januari 2015 hadi Machi, 2018 baada ya kukosa ndugu.
 
Miili hii ilichukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali za rufaa za Temeke, Mwananyamala, Amana, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na hospitali ya Vijibweni.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na katibu wa Afya wa Halmashauri ya Jiji, Benson Mallya, mwaka 2015 mamlaka hiyo ililazimika kuzika miili ya watu 371 baada ya kutojitokeza ndugu wa kuizika wala watu walioidai.
 
Idadi hiyo ilipungua kidogo mwaka 2016 wakati halmashauri hiyo ilipopokea miili ya watu 334 kutoka hospitali mbalimbali kwa ajili ya kuzika.

Mwaka jana 2017 idadi hiyo iliongezeka kwa kiasi kikubwa baada ya miili ya watu 447 kuruhusiwa kuzikwa na mamlaka hiyo ya jiji.
 
Takwimu ambazo Mwananchi limezikusanya katika hospitali ya Muhimbili, Temeke na Mwananyamala pekee zinaonyesha kuwa maiti 690 zilizikwa kwa mtindo huo kati ya Januari 2015 na Desemba 2017.

Kwa kipindi hicho, Hospitali ya Muhimbili imetoa takwimu zinazoonyesha kuwa walilazimika kuruhusu miili 259 izikwe na jiji kwa kukosa ndugu.
 
Katika Hospitali ya Mwananyamala, takwimu zinaonyesha kuwa miili 188 iliyokosa watu wa kuidai na iliidhinishwa kuzikwa na jiji wakati Hospitali ya Temeke iliruhusu miili 243 izikwe na jiji kwa kipindi hicho hicho.

Wanatoka wapi?

Pengine swali linaweza kuwa sababu za miili hiyo kukosa ndugu au jamaa wa kuihifadhi kwa taratibu na heshima kama ilivyo kwa maiti nyingine.
 
Katika hali ambayo takriban asilimia 70 ya magari yote yanayoingia nchini yanatumiwa jijini Dar es Salaam, huwezi kuacha kufikiria kuwa ajali za barabarani zinaweza kuwa chanzo kikuu cha maiti zinazokosa ndugu au kutotambuliwa.

“Ajali za barabarani ndio chanzo cha vifo kwa maiti nyingi zinazokosa ndugu,” alisema ofisa uhusiano wa Muhimbili, Aminieli Eligaesha.
 
Anasema wamo pia watu wanaouawa baada ya wananchi kujichukulia sheria mkononi, wanaozama baharini na wachache wanaookotwa kwenye fukwe za bahari.

Katibu wa afya wa Halmashauri ya Jiji, Benson Mallya, anasema maiti nyingi zisizokuwa na ndugu ni za watu masikini ambao hufika Dar es Salaam kama wafanyabiashara ndogondogo au ombaomba na kufikwa na mauti bila ndugu wa karibu kuwa na habari.
 
Back
Top Bottom