Miili hii ilichukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Hospitali za rufaa za Temeke, Mwananyamala, Amana, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) na hospitali ya Vijibweni.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na katibu wa Afya wa Halmashauri ya Jiji, Benson Mallya, mwaka 2015 mamlaka hiyo ililazimika kuzika miili ya watu 371 baada ya kutojitokeza ndugu wa kuizika wala watu walioidai.