Majimaji hurahisisha mpepeso wa kope na wakati huo huo huzikinga kope hizo zisigandane pale zinapofumba. Wakati wa kulala, ni muhimu kwa kope kufumbika. Laiti kope zisingeliyafumba macho, basi ulalaji ungelikuwa wa maumivu na wa tabu. Ingelibidi mtu aishi katika chumba cha giza wakati wote, asikutane na mwanga.