Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwa kukosa kope, jicho ambalo sasa lingelikuwa halina kinga hata ya kuzuia hatari ndogo tu, mara zote lingekuwa katika hatari ya kupofuka.
Ukiwa ni mfano hai hebu tazama ugonjwa wa vikope (lagophthalmos) ambapo wanaougua ugonjwa huo hushindwa kufumba macho sawasawa. Uambukizo pamoja na kukauka kwa konea, huwa ni mambo yasiyoweza kuepukika.
 
Matatizo sugu huweza kutokea kutokana na kuharibika kwa jicho. Kwa kuwa kope haziwezi kufumbika sawasawa na kwa kuwa majimaji ya kusafishia hayapo, mgonjwa huhitajika muda wote kusafisha na kuyatia macho dawa ya kuyakinga na maambukizi.
Zaidi ya hivyo, jicho linalobaki bila kufumba vizuri usiku kucha hukusanya uchafu kwa njia ya hewa na vumbi hadi kufika asubuhi.
 
Matatizo sugu huweza kutokea kutokana na kuharibika kwa jicho. Kwa kuwa kope haziwezi kufumbika sawasawa na kwa kuwa majimaji ya kusafishia hayapo, mgonjwa huhitajika muda wote kusafisha na kuyatia macho dawa ya kuyakinga na maambukizi.
Zaidi ya hivyo, jicho linalobaki bila kufumba vizuri usiku kucha hukusanya uchafu kwa njia ya hewa na vumbi hadi kufika asubuhi.
 
Mfumo wa Kutoa Tahadhari Mapema

Jicho hukingwa kwa msaada wa Mfumo uliojengeka kutoa tahadhari mapema. Pale hatari inapotishia jicho, neva hufanya kazi ya kuzishughulisha kope, kuhamasisha misuli inayozifumba kope.
 
Kubwenza-bwenza (blinking)
v Kujifumba zenyewe kimaumbile (relflex)
v Kuzifumba kwa hiyari (consciously)
Kubweza ni dhamana ya vipingili vinavyoshikilia jicho na ambavyo huishi kwa mawasiliano na angahewa. Kwa wanadamu, kiwango cha ubwenzaji wa macho ni baina ya kumi hadi ishirini kwa dakika moja kutegemeana na shughuli kama vile kusoma na kuelekeza mazingatio makubwa katika kile unachosoma pamoja, na hali kama vile ongezeko la umande zote hizi hupunguza kasi ya ubwenzaji wa macho.
 
Katika mwanga mkali, kasi ya ubwenzaji macho huongezeka. Hivyo basi, afya ya macho hudumishwa na kasi ya ubwenzaji wa macho yenyewe, ikituondosha katika hali ya usumbufu wa kulazimika kuyafumba sisi wenyewe kila yanapokabiliwa na hatari.
 
Kope kujifumba zenyewe (reflex) ni kitendo kisichokuwa cha hiyari na cha haraka kinachotokana na misukumo mbalimbali. Kuna mtambo unaozifanyisha kazi kope pasipo hiyari yetu ili kulikinga jicho na hatari za nje.
Uchunguzi wa ndani wa mtandao wa mishipa inayoendesha matendo yasiyo ya hiyari ya jicho unabainisha mpangilio maridadi usio na dosari wa kazi ya usanifu.
 
Kwa kila kitendo kisicho cha hiyari, jumbe mbalimbali hutoka katika njia mbalimbali za mishipa. Maeneo ya jicho huzingirwa na mitandao ya tahadhari za mapema.
Ubongo, baada ya kutathmini tahadhari hizo zinazosafiri haraka, hupeleka jumbe katika misuli inayohusika, ukizielekeza njia jumbe hizo kule ziendako bila kukosea katika mtandao wenye mvurugano-mvurugano.
 
Ndani ya sekunde, sigino ya tahadhari huufikia ubongo na kurejea kama amri, kwa amri hiyo, kope huwahi hufumba, kukinga na kusafisha duara la jicho.
Mchakato wa kutambua hatari na kutengeneza kinga tofauti za matendo yasiyo ya hiyari kwa njia ya sigino zinazosafiri katika njia mbalimbali za mishipa, ni tete mno.
 
Kuzitambua Neema za Mwenyezi Mungu

Kubwenza ni kitendo kisicho cha hiyari ambacho hufanyika mara elfu nyingi kila siku. Hakuna mtu anayehangaika kubwenza, hakuna mtu anayeamua wakati gani abwenze na wakati gani asibwenze.
 
Bila shaka, yapo magonjwa ya kope za macho. Moja ya magonjwa mashuhuri ni ule unaosababishwa na udhaifu wa misuli inayonyanyua kope ya juu ya jicho. Kwa hali hiyo, kope moja au zote mbili hubakia chini na kufanya uso upooze, uonekana kama vile mtu ana usingizi.
 
Ni jambo la kuajabisha kuwa misuli hiyo hiyo ya kope ambayo huweza kuonekana kwa hadubini tu, hufanya kazi bila kuchoka katika maisha yetu yote, na aghalabu nje ya udhibiti wetu. Waumini wa Mungu wanaposoma mambo haya imani yao huzidi.
 
Back
Top Bottom