Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

30945396_124471008412997_4226451250389975040_n.jpg
 
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema watumishi 22 wa Taasisi ya Elimu Tanzania wamesimamishwa kazi kwa kuisababishia Serikali hasara ya kuchapisha vitabu vyenye makosa.

“Kuna watumishi 22 wa Taasisi ya Elimu wamesimamishwa kazi na hatutaishia kuwasimamisha kazi tu, bali kuangalia hatua za kuwachukulia kwa sheria zipi zitahusika kwani wameisababishia Serikali hasara.”
 
Profesa Ndalichako alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Felister Bura bungeni mjini Dodoma leo Mei 2, wakati Bunge likiwa limekaa kama kamati kupitisha bajeti ya wizara ya elimu ya mwaka 2018/19.

Katika majibu yake, Profesa Ndalichako amesema ni kweli kuna makosa katika vitabu hasa baada ya wabunge kuliibua bungeni mwaka jana.
 
Hata vitabu mlivyosema ni vichache, tulivyopitia tulibaini vitabu 16 na tumevifanyia mabadiliko vya kuanzia darasa la kwanza, pili, tatu na nne na tumesimamia vyema kuchapwa upya,” amesema Profesa Ndalichako.
 
. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani kwa siku tano mfululizo zinazoweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TMA, mvua hizo zimeanza jana Mei Mosi na zitaendelea mpaka Mei tano mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja.
 
. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kunyesha mvua kubwa juu ya wastani kwa siku tano mfululizo zinazoweza kusababisha mafuriko katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na TMA, mvua hizo zimeanza jana Mei Mosi na zitaendelea mpaka Mei tano mwaka huu na zinatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga pamoja na visiwa vya Pemba na Unguja.
 
Mikoa mingine itakayoathirika na mvua hizo ni Mara, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Tabora, Katavi, Kigoma, Arusha, Kilimanjaro na Manyara.

TMA imesema kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni pamoja na mafuriko katika baadhi ya maeneo na kuathiri jamii, adha ya usafiri kwa barabara kubwa kutopitika.
 
Kwa mujibu wa TMA athari za mvua hizo ni kujaa kwa maji au yanayopita kwa kasi na kuhamishwa kwa watu kutoka maeneo yaliyoathiriwa.

Angalizo lingine ni upepo mkali na mawimbi makubwa kwa maeneo ya ukanda wa Pwani inayojumuisha mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara pamoja na Visiwa vya Pemba na Unguja.
 
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wameshtushwa na mapato ya utalii yanayokusanywa katika visiwa vya Bongonyo na Mbudya, hivyo kutaka uwekezaji mkubwa zaidi ufanyike kuboresha mapato ya ndani.

Hamasa hiyo imejitokeza mwishoni mwa wiki iliyopita, baada ya madiwani hao kutembelea visiwa hivyo na kupokea ripoti ya mapato kwa miaka mitatu mfululizo.
 
Mhifadhi wa maeneo tengefu ya Dar es Salaam, Anita Julius aliwaeleza wajumbe hao wa baraza la madiwani la jiji kuwa mwaka 2015, watalii 14,708 walitembelea visiwa hivyo na kuingiza Sh280 milioni wakati mwaka 2016 watalii 37,675 walifika na Sh415 milioni zilipatikana na kuanzia mwaka 2017 mpaka Machi, Sh280,000 milioni zilikusanywa.
 
Diwani wa Mwananyamala, Songoro Mnyonge alisema visiwa hivyo ni sehemu nzuri ya kuongeza mapato kwa Dar es Salaam.

“Ipo haja ya kuvitangaza vituo hivyo ili vijulikane. Naamini wakazi wengi wa Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla hawavijui,” alisema Mnyonge.

Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Issaya Mwita aliyeongoza msafara wa madiwani hao alisema ipo haja ya kuvichukulia kwa uzito visiwa hivyo na kuahidi kuimarisha usafiri wa kufika maeneo hayo ili kuwaruhusu wananchi wengi zaidi kuvitembelea.
 
Back
Top Bottom