Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Waziri Mkuu apiga marufuku kupandisha bei

MUUNGWANA BLOG / 17 minutes ago




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapiga marufuku wafanyabiashara wote nchini kupandisha bei ya sukari pamoja na bidhaa nyingine katika kipindi ambacho waumini wa kiislamu wanakuwa katika ibada ya kufunga mwezi wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza siku si nyingi kutoka sasa ndani ya mwezi huu Mei.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 03, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la nyongeza la Mbunge Abdallah Bulembo aliyetaka kusikia tamko la serikali juu ya tatizo la sukari kuelekea mwezi wa ramadhani

"Suala la sukari tumelitafutia ufumbuzi tukiwa tunalenga kwanza upatikanaji wa bidhaa yenyewe iwe ya kutosha na kila mwenye mahitaji ya matumizi ili aweze kuipata sukari kwa urahisi ikiwemo na waislamu wanaoanza kufunga mwezi wa Ramadhani siku chache zijazo. Tunajua kila mwaka huwa tuna upungufu wa sukari lakini utaratibu tunaotumia ni kutoa vibali vya kuingiza sukari nchini ili kuweza kufanya soko la sukari kuendelea kuwepo na kufanya hivyo inasaidia hata bei za ndani kupungua"

Waziri Mkuu ameendelea kusema

"Kwa hiyo nataka niwaondolee mashaka watanzania na hasa waislamu kama ambavyo Mhe. Bulembo amesema kwamba sukari itapatikana kipindi chote cha ramadhani na maeneo yote ambayo yanahitaji sukari, pia tutaendelea kufuatilia muenendo wa bei ili watu wasiweze kupandisha bei ya sukari kwa makusudi tu kwa sababu watu wanajua mahitaji ya sukari yatakuwa makubwa kwa kufunga ramadhani".

Pamoja na hayo, Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema "hili nalo tutalifanyia ufatiliaji kwenye maduka kwa sababu tumeweka utaratibu kusiwe na mtu yeyote anayeweza kupandisha bidhaa ya aina yeyote ile wakati wa ramadhani kwasababu kwa kufanya hivyo atakuwa anawaadhibu waislamu ambao wanaofunga ramadhani kwa sababu tu mahitaji yanakuwa makubwa".

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema wameilekeza TRA vizuri kuwa wasitumie nguvu wala lugha chafu katika kukasanya kodi kwa wafanyabiashara nchini na kuwataka wafanyabiashara wote wawe na amani katika kufanyakazi zao pamoja na wawekazaji.
 
14723571_328896237488747_9107530115977314304_n.jpg
 
Wabunge wameitaka Serikali kuchukua hatua ikiwamo kuwataka wanasiasa walioonekana wakiwachoma sindano ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi, kuomba radhi na kuwalipa fidia watoto hao.

Hata hivyo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kilichofanyika ni majaribo huku akikiri kushika sindano kama si mtaalamu ni makosa.
 
Mabosi wa kampuni iliyomtapeli Mzee Majuto mamilioni wadakwa na Polisi

MUUNGWANA BLOG / 18 minutes ago




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa kuna Kampuni iko Mwanza iliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa, Hivyo serikali imewachukulia hatua wahusika.

“Naomba niwaeleze wananchi Nimeunda jopo la wanasheria na tumeshaanza kikao cha kwanza sasa hivi kazi yetu kubwa kwasababu tumeshaanza na suala la Mzee Majuto ni kuangalia kazi zote alizokwisha zifanya na tunawaandikia barua wote waliohusika watupe mikataba wanayoijua wao tutakaa nao tuanza kuchambua mkataba mmoja baada mwingine na tutawataarifu itakavyo fuatia,” amesema Dkt. Mwakyembe

“Kuna kampuni moja ya Mwanza waliingia Mkataba na King Majuto na Mkataba huo ulikuwa ni wakumlipa Milioni 24 wakatoa check, check hiyo ikawa haina Pesa tunashukuru uongozi wa Mwanza kwa kushirikiana nao wahusika wako ndani na tutaendelea kuchukua hatua kali kwa watu ambao wanadhani wanaweza kutumia jasho la wenzao kujinufaisha wenyewe,” alisisitiza.
 
Hayo yamejitokeza leo Mei 3, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati wabunge wakiomba mwongozo wa Spika, wakitumia kanuni ya 67 (8) ya jambo lililotokea hivi karibuni.

Aliyeanzisha alikuwa mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Anatropia Theonest aliyehoji kuwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, wamejitokeza madaktari wa ghafla wakiwamo wakuu wa wilaya na wabunge, wakichanja watoto.
 
Sasa nimepata taharuki, sisi kama hatuna taaluma, tunachomaje sindano, nimesikia waziri ametoa kauli lakini haitoshi, nimesoma miiko ya madaktari hairuhusu, nimesoma miiko ya wauguzi hakuna,” amesema.

Katika kusisitiza hilo, Theonest amesema; “Madaktari wamevunja miiko, wauguzi wamevunja miiko na wanasiasa hao wamevunja maadili yao. Naomba hao watu waliochoma sindano wawaombe radhi na watoto wapewe fidia na mabaraza husika yanachukua hatua gani katika hilo?
 
Mrithi wa Morgan Tsvangirai: Mkinichagua kuwa Rais nitawafukuza Wachina wote

MUUNGWANA BLOG / 19 minutes ago




Kiongozi wa chama cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC) nchini Zimbabwe, Nelson Chamisa amesema kuwa atawafukuza wawekezaji wote kutoka China nchini humo endapo atachaguliwa kuwa Rais kwenye uchaguzi mkuu mwezi Julai mwaka huu.

Chamisa amesema kuwa Wachina wamekuwa wakitorosha rasilimali za nchi hiyo na uwekezaji wao umegubikwa na rushwa hivyo haoni sababu ya kuwaruhusu kufanya kazi nchini humo.

“Wawekezaji kutoka china ni moja ya watu wanaolifilisi taifa letu, wanachukua rasilimali zetu kwa kisingizio cha uwekezaji na wamesaini mikataba ya hovyo na serikali ya Zanu-PF sioni umuhimu wao ni bora tukaacha hizo rasilimali zikatumiwa baadae nawaahidi mkinichagua kuwa rais nitawafukuza wawekezaji wote Wachina na wengine ambao wataonekana na mikataba kama hiyo nitawatimua, tumechoka kunyonywa,“amesema Chamisa juzi Mei 01, 2018 mjini Harare kwenye maadhimisho ya siku yawafanyakazi duniani.

Zimbabwe inatajwa kuwa ni nchi ya nne barani Afrika kuwa na wawekezaji wengi kutoka China, na hoja hiyo inaungwa mkono na wabunge wengi hata wale wa chama tawala cha ZANU-PF.

Uchaguzi huo mkuu utakuwa uchaguzi wa kwanza na wa kihistoia nchini humo tangu utawala wa Robert Mugabe kuangushwa mwezi Januari mwaka huu.

Chamisa alitangazwa kuwa kiongozi wa chama cha MDC mwezi Februari akimrithi aliyekuwa kiongozi wa chama hicho, Morgan Tsvangirai baada kufariki dunia.

Mpinzani mkubwa wa Chamisa ni Rais wa sasa wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa maarufu kwa jina la ‘Ngwena’ yaani MAMBA .
 
Waziri Mkuu atoa onyo kali kwa TRA

MUUNGWANA BLOG / 20 minutes ago




Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameionya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuacha kutumia lugha zenye kuudhi wananchi pindi wanapokwenda kukusanya kodi kwa wafanyabiashara katika maeneo yao ya kazi pamoja na kutowatoza kodi kubwa ambayo haina uhalisia.

Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 03, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge rank Mwakajoka aliyetaka kujua Serikali inatoa kauli gani kuhusu matatizo wanayofanyiwa wafanyabishara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

"Wafanyabiashara wote kwanza wawe na amani katika kufanyabiashara zao nchini na wawekezaji wote waendelee kuwekeza na kuongeza mtaji zaidi ili kuekeza zaidi kwa sababu serikali imedhamiria kufungua milango ya uwekezaji nchini. Tunajua kwamba kodi ni wajibu wa kila mmoja kadiri ya shughuli zake zinazomletea mapato ilivyo kwa ukubwa wake. Kwa hiyo tumeielekeza TRA ihakikishe inapokwenda kukusanya kodi haitumii lugha ya kuudhi wala nguvu", amesema Majaliwa.

Pamoja na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "ndio maana tulianzisha kitengo cha elimu ndani ya TRA ikiwa na lengo la kumuelimisha mwananchi umuhimu wa kulipa kodi, hakuna sababu ya kumlazimisha mlipa kodi. Pale patapotokea malalamiko wafanyabiashara wana uhuru mkubwa wakuenda kwa kiongozi mkubwa wa eneo hilo ili kulalamikia jambo hilo ili sheria zipate kuchukuliwa".

Kwa upande mwingine, Waziri Majaliwa amesema serikali haina ugomvi na wafanyabishara na TRA wanapaswa kufanya kazi vyema huku akiwaomba wafanyabiashara kutoa taarifa pindi wanapobughudhiwa na TRA wasiwapandishie, kodi wafanyabiashara.
 
Mbunge mwingine wa Viti Maalum (Chadema), Anna Gidarya alimuunga mkono Theonest akisema; “Huwezi kwenda tu kumchoma, chanjo ndizo zinaleta matatizo hata sisi wataalamu tunajua.”

Akitoa majibu ya miongozo hiyo, Spika Job Ndugai amesema, “Tunawaachia Serikali walifuatilie.”
 
Waziri Mwalimu alijibu miongozo hiyo akisema;

“Nakiri, uchomaji wa sindano una taratibu zake, huwezi kujichomea ovyo ovyo, nawahakikishia Mshana na Mlinga hawakuwachoma chanjo watoto husika ila walifanya kama majaribio.”

Mwalimu amesema ametoa maagizo kwa waganga wa mkoa na wilaya na kuwaeleza kuwa hata kushika sindano ni makosa.
 
Back
Top Bottom