Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtoto wa kiume akikosa simulizi za maisha kutoka kwa mama mzazi/mlezi,matokeo yake ndio hayo.
Thamani ya mwanamke haijawahi kubadilika ila umuhimu ndio hutofautiana. Mama ni muhimu sana, ila ana thamani sawa na wanawake wote, tuwathamini, tuwa heshimu na ikibidi tuwapende hata kwa kuji lazimisha.

"ukitaka kukosa likes zangu jisifie umempiga 'kishenzi' mwanamke wako"
 
[emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Dah! Aisee[emoji23][emoji23]
 
NI HUKO AFRIKA YA KUSIN

MCHUNGAJI WA KANISA LA KIPENTEKOSTE AMESEMA KUWA NI RAHISI KUFANYA NGONO NA WASICHANA WANAOKWENDA KANISANI KULIKO AMBAO HAWAENDI KANISANI.

Mchungaji wa Kanisa la Kipentekoste huko Afrika Kusini amesema kuwa ni rahisi sana kwa mhubiri kufanya ngono na wasichana wanaokwenda kanisani kuliko ambao hawaendi kanisani.

Mchungaji Benard Pumalaka amesema hayo Jumatano moja huko Afrika kusini baada ya kuokoka.

Amesema kuwa wengi wanaojiita "Manabii" ni maarufu kwa ngono na wasichana na wake za watu.

Bernard alisema "kabla sijawa mchungaji wa Pentekoste, nilikuwa nimelala na watu wawili tu-mke wangu, na mwanamke mwingine mmoja tu.

Lakini nilipopata uchungaji nimelala na wanawake zaidi ya 200 ktk miaka kumi! Na nimepata utajiri mkubwa kwa kuwadanganya waumini wangu.

Nimejipatia fedha nyingi,magari na nyumba kwa kuwahadaa waumini wangu.Hakika sikuwa na Yesu ndani mwangu."

Mchungaji huyu aliyeokoka aliendelea kusema " Nawaeleza kuwa ni rahisi sana kwa nabii kuhadaa na kulala na wasichana wanaokwenda kanisani kuliko wale ambao hawaendi.

Ni rahisi kuwaibia waumini kuliko wasio waumini.

Ndo sababu utakuta wengi wa waumini ni maskini, lakini Nabii au Mchungaji au Askofu wao ni tajiri wa kupindukia."

Mchungaji Pumalaka aliendelea kusema " wanawake wengi huja kanisani kwa sababu ya shida zao na wala sio kuabudu.

Wanakuja kuomba utajiri au kuponywa magonjwa au kutafuta wachumba au kuomba kizazi na kadhalika.

Kwa bahati mbaya sisi Manabii tunachukua udhaifu na shida zao kuwatapeli pesa zao na kufanya nao ngono.

Lakini mimi leo nimeamua kutangaza hadharani kuwa nimeokoka na nitamtumikia Mungu wa kweli"
Mwishowe, Mchungaji Pumalaka alisema "Nawaambieni kuwa yeyote anayehubiri utajiri, fedha, kazi nzuri, afya tele nk. ni mwongo.

Nabii wa kweli anahubiri wokovu tu. Ni baada ya wokovu vitu hivi vingine vitakuja.

Yesu, Simon Petro, Paulo Daniel, Isaka na maelfu ya watu wa Mungu walihubiri wokovu tu, na wala siyo utajiri au miujiza."

Baada ya kusema haya,mchungaji Pumalaka aliwaeleza waumini kuwa 95% ya wanaojiita Manabii ni Matapeli tu.

Wanatumia nguvu za Shetani kuwaibia na kufanya ngono na waumini wao. Aidha 98% ya manabii hawana lolote bali ni bandia(fake) tu.

Baada ya kuungama, mchungaji Benard Pumalaka aliwatangazia waumini wake kuwa atauza mali zake zote na kuwagawia maskini na Kanisa. Alimalizia kwa kusema "ni bora kuwa maskini hapa duniani lakini tajiri huko mbinguni"..

Sent as Received.
 
NSSF yataja aina ya wanachama litakaohudumia

Muungwana Blog 5 · 53 minutes ago




SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), limetaja aina ya wanachama litakaohudumia baada ya Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kusainiwa na Rais John Magufuli hivi karibuni.

Meneja Kiongozi wa NSSF Mkoa wa Temeke, James Oigo, aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waajiri kuhusu sheria hiyo mpya na wajibu wao katika kulinda haki za wanachama.

Watu watakaokuwa wanachama wa NSSF, alisema, ni waajiriwa wote wa sekta binafsi, wageni ambao wameajiriwa Tanzania Bara, waajiriwa katika taasisi za kimataifa zinazofanya kazi Tanzania Bara na watu wote waliojiajiri wenyewe na wale wa sekta isiyo rasmi.

Kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya mwaka jana, mifuko ya sekta hiyo imeunganishwa na kubaki miwili - NSSF na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).

Mifuko iliyounganishwa kwa sheria mpya ni PPF, GEPF, LAPF na PSPF.

Oigo alisema NSSF inawatembelea wanachama wake nchi nzima kuwaelimisha juu ya sheria hiyo, ili kuondoa hofu iliyopo miongoni mwao baada ya mifuko kuunganishwa na kubaki miwili.

Katika ziara hizo, alisema, NSSF itahimiza waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi kwa wakati ili kuliwezesha shirika kulipa mafao ya wanachama kwa ufanisi, kuzijua changamoto zinazowakumba waajiri.

"Waajiriwa wote ambao wataajiriwa baada ya sheria hii kuanza ndio watakuwa katika mfuko ama wa PSSSF endapo wanaajiriwa katika sekta ya umma na NSSF endapo wanaajiriwa katika sekta binafsi," alifafanua.

Aidha, alisema waliokwishaajiriwa wakati sheria hiyo inaanza ambao walikuwa katika mifuko iliyounganishwa watakuwa wanachama wa mfuko wa PSSSF bila kujali wapo setka binafsi au ya umma.

Aidha, watumishi ambao walikuwa wanachama wa NSSF watabakia kuwa wanachama wa NSSF bila kujali sekta wanayotoka, alisema Oigo.

Alizidi kufafanua kuwa kanuni ya ulipaji mafao na idadi ya mafao yatakuwa ya aina moja kwa mifuko yote miwili.

Akifungua mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji wa NSSF, Bathow Mmuni, alisema sheria mpya ya hifadhi ya jamii imeshasainiwa na Rais na sasa zimebakia taratibu za kiuendeshaji.

Naye Meneja wa NSSF Kinondoni, Marco Magheke, alisema shirika limejipanga kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wanachama wake.
 
Zijue sababu za Watoto kukosa Hamu ya kula Chakula
Muungwana Blog 2 · 15 minutes ago


Kukosa hamu ya kula ni tatizo la kawaida kwa watoto ambalo hupelekea wazazi wengi kuwa na wasiwasi juu ya afya ya watoto wao. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kukosa hamu ya kula na tatizo hili linapojitokeza tunatakiwa kuwa watulivu na kujaribu kuchunguza kwa makini ni kwa nini mtoto anakosa hamu ya kula. Baadhi ya sababu zaweza kutatuliwa na mzazi au mlezi lakini sababu nyingine kama zisababishwazo na magonjwa zitahitaji msaada wa wataalam wa afya.

Moja ya sababu kubwa ambayo huwakosesha watoto hamu ya kula ni aina mbalimbali za magonjwa. Magonjwa kama Malaria, kuhara, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa, magonjwa ya kinywa na koo, homa na mafua au dalili nyinginezo ambazo humkosesha mtoto raha hupelekea watoto kukosa hamu ya kula.

Matatizo ya kifamilia na msongo ni sababu nyingine ambayo huwakosesha watoto raha na hamu ya kula. Kama walivyo watu wazima watoto pia hukumbana na matatizo ya kifamilia kama kupoteza ndugu au vitu wavipendavyo. Lakini pia watoto hukumbana pia na changamoto mbalimbali za kimaisha kama majukumu ya shule au pengine kukumbana na unyanyasaji kama kuzomewa na mambo mengine mengi yanayokiuka haki zao.

Kwa hiyo ili kumuepusha mtoto na ukosefu wa hamu ya kula, wazazi na walezi hawana budi kuwa makini endapo wataona mabadiliko yoyote ya kitabia ya mtoto. Kugundua na kuweza kuziondoa sababu zinazomsababishia mtoto msongo, tutaweza kuwarudisha katika hali ya kawaida na hamu ya kula itarejea tena.

Lakini pia wakati mwingine hali hii hutokana na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula ujulikanao kitaalam kama Anorexia nervosa. Watoto wenye ugonjwa huu huweza kukaa muda mrefu bila kula ingawa hawana tatizo jingine, na endapo watapewa chakula huchagua aina fulani tu ya chakula jambo ambalo hupelekea kutopata mlo ulio kamili na hii hupelekea kupungua uzito pamoja na kudhoofu kwa afya zao .

Jambo hili linapojitokeza ni vyema kumpeleka mtoto kwa wataalam wa afya wa masuala ya lishe ambao watakuwa msaada mkubwa katika kumsaidia mtoto wako kurejesha tena hamu ya kula.

Kiwango kidogo cha ukuaji wa mtoto huchangia kupungua kwa hamu ya kula. Katika mwaka wa kwanza wa maisha ya watoto, watoto hukua haraka lakini baada ya mwaka mmoja kiwango cha ukuaji hupungua na kiwango cha chakula wanachokula pia hupungua. Katika wakati huo, hali hiyo ni ya kawaida katika maisha ya watoto.

Sababu nyingine ambazo huchangia watoto kukosa hamu ya kula ni kama maudhi ya dawa, upungufu wa damu, uambukizi wa minyoo na matatizo ya mmeng'enyo mfano mtoto kutopata choo.

Maudhi ya dawa mbalimbali ambazo hutumika kutibu magonjwa kwa watoto yanaweza kuchangia watoto kukosa hamu ya kula. Mfano daktari akimwandikia mtoto dawa za antibiotiki, zaweza kusababisha tazizo la kukosa hamu ya kula. Kupoteza hamu ya kula kwa watoto wanaotumia antibiotiki ni maudhi ya dawa ambayo huwapata watoto wengi. Dawa nyingine pia zaweza kupelekea kupata maudhi ya dawa kama kichefuchefu na kutapika. Tatizo hili humalizika mtoto anapomaliza dawa na endapo atakuwa amepona.

Uambukizi wa minyoo huchangia tatizo hili. Minyoo huingia katika mfumo wa mmeng'enyo wa watoto na kusababisha upotevu wa damu. Minyoo hutegemea ufyonzaji wa damu kama chakula chao, na katika uambukizi sugu hupelekea kuvuja kwa damu,upungufu wa damu, kuhara, kichefuchefu, kutapika na kukosa hamu ya kula. Endapo mtoto ataonyesha dalili za umbukizi wa minyoo, ni vyema kuwaona wataalam wa afya ili kuweza kufanyiwa vipimo na kupatiwa matibabu.

Ugonjwa wa upungufu wa damu ambao kwa kitaalam hujulikana kama anemia, husababishia watoto tatizo hili. Kiwango kidogo cha madini ya chuma katika damu, huwapata watoto ambao hawapati lishe ya kutosha yenye madini haya. Lakini pia anemia yaweza kusababishwa na uambukizi wa minyoo au hata magonjwa mengine. Watoto wenye anemia huwa wadhaifu na wasio wachangamfu, na kama ugonjwa usipotibiwa utaathiri afya ya mtoto hata maendeleo yake shuleni. Ni vyema mtoto akafanyiwa vipimo vya damu endapo utahisi au ataonyesha dalili za ugonjwa wa anemia.

Kwa watoto ha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…