Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mlela afunguka Mzee Majuto kuomba msaada ni udhalilishaji mkubwa.

MUUNGWANA BLOG / 3 hours ago




Muigizaji wa filamu Bongo Yusuph Mlela, amesema kitendo cha Mzee Majuto kuomba msaada kwa watu mbali mbali ili aweze kwenda kupata matibabu,ni udhalilishaji mkubwa.

Mlela ameyasema hayo kwenye eNewz ya East Africa Television, na kueleza kwamba wao kama wasanii wanatakiwa wajifunze, kwani kitendo cha msanii mkubwa kama yule kukosa matibabu kwa kutokuwa na pesa sio kitu sahihi na inaonesha ni jinsi gani wasanii wako chini kiuchumi, licha ya kazi nyingi na matangazo mabli mbali ambayo amewahi kuyafanya.

“Kiukweli si sahihi inanionesha ni jinsi gani bado tuko chini, kuomba msaada vile ni udhalilishaji, sisi ambao tuko kwenye game na umri unaruhusu tuchukulie kama changamoto tujipange kama binadamu, haya yasiendelee kujitokeza”, amesema Yusuph Mlela.

Kutokana na hilo Yusuph Mlela ameitaka serikali kutia mkono wake na kusimamia haki na kazi za wasanii, ili waweze kuingiza kile ambacho wanakitolea jasho kwa usahihi.
 
31028388_184311082197634_2818093171513229312_n.jpg
 
Kabwili aiacha Ngorongoro Heroes

ShaffihDauda / Dick Dauda / 7 hours ago

Wakati timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20 ‘Ngorongoro Heroes’ ikijiandaa kwa ajili ya mchezo wake dhidi ya Mali kuwania kufuzu fainali za Afrika, golikipa namba moja wa timu hiyo Ramadhani Kabwili hatokuwa sehemu ya kikosi kitakachocheza mchezo wa kwanza Dar.

Kocha wa Ngorongoro Heroes Ammy Ninje amesema Kabwili atakuwa na majukumu kwenye klabu yake ya Yanga hivyo watafanya maboresho katika eneo hilo.

“Tutafanya maboresho kwenye eneo la golikipa kwa sababu Kabwili hatokuwa na sisi atakuwa kwenye majukumu na Yanga, tuna golikipa mmoja tutamleta mwingine kutoka Zanzibar kwa hiyo ni eneo hilo tu ndio litafanyiwa maboresho.”

“Golikipa kutoka Zanzibar namfahamu kwa jina moja tu Seif anatoka JKU, akija tutam-assess atajiunga na sisi.”

“DR Congo ilikuwa timu ngumu lakini tulifanikiwa kuwatoa, tunaheshimu timu zote ambazo zipo kwenye mashindano lakini kitu muhimu ni matayarisho. Tukifanya matayarisho na wachezaji wangu wakachukua misingi tuliyopeana basi mechi inaweza kuwa rahisi.”

“Kwenye timu yoyote hayawezi kukosekana makosa ndiyo maana tunafanya marekebisho. Wachezaji wanajituma vizuri uwanjani wanafuata maelekezo tunayowapa na unaona kila mchezaji ana hamu ya kuanza.”

Visit website
 
“Nchi hii haimuoni Mkude? Au kwakuwa hachani nywele?” Haji Manara

ShaffihDauda / Dick Dauda / 8 hours ago

Ofisa habari wa klabu ya Simba Haji Manara kupitia ukurasa wake wa instgram ame-post ujumbe amihoji maswali kadhaa kuhusu Jonas Mkude kuchukuliwa poa Tanzania.

Manara amehoji kwamba nchi hii haimuoni Jonasi Mkude? Tatizo ni jina lake la Kiluguru au kwa kuwa hachani nywele? Halafu mwisho amesema kwa sasa hakuna mbadala wake nchini.

Ujumbe huo ame-post Jumatano Mei 2, 2018 unasomeka hivi:

“Leo nimekaa nikajiuliza swali moja gumu kisha nikakosa majibu…hivi nchi hii haimuoni Jonas Mkude? Tatizo ni nini au hilo jina lake Mkude limekaa Kiluguru sana au kwa kuwa hachani nywele? Huyu jamaa amezaliwa midfielder na kwa sasa akuna mbadala wake kwenye nchi hii ya JPM.”

“Please jamani tuwe serious na vipawa vya watu.”

Manara aliwahi kuhoji pia kuachwa kwa Mkude kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichotajwa kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki za kalenda ya Fifa dhidi ya Algeria na DR Congo.

Visit website
 
Liverpool haooo wanakwenda Kyiv

ShaffihDauda / Kicki_19 / 16 hours ago

Pamoja na kipigo cha mabao 4-2 kutoka kwa As Roma, lakini Liverpool wamefanikiwa kufudhu kwenda fainali ya michuano ya Champions League kwa aggregate ya mabao 6-7, na hii ikiwa ni fainali yao ya 8 wanakwenda.

Roberto Firminho alitoa assist iliyozaa bao la kwanza la Liverpool lililofungwa na Sadio Mane, assist ya Firminho inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza katika miaka 10 ya mwisho ya CL kuwahi kuwa na walau mabao 7 na assist 7 katika msimu mmoja wa CL.

Dakika ya 15 ya mchezo, As Roma walipata bao baada ya James Milner kujifunga. Hili linakuwa bao la kwanza kwa Liverpool kujifunga tangu Johne Arne Riise ajifunge katika mchezo wa nusu fainali vs Chelsea msimu wa 2007/2008.

Dakika ya 25 Liverpool walipata tena bao la kuongoza kupitia kwa Gerginio Wijnaldum, na hili likiwa bao la 19 kwa Wijnaldum kuwahi kuzifungia timu za Uingereza, 11 akiwafungia Newcastle na 8 akiwafungia Liverpool.

Bao la Mane limeufanya utatu wa Liverpool kufikisha jumla ya mabao 29 katika Champions League msimu huu, sasa Mane, Salah na Firmino wanakuwa wamefunga mabao mengi kuliko Bale, Benzema na Cr7 walivyofunga msimu wa 2013/2014 (28).

Bao la leo la Edin Dzeko linamfanya kufunga mabao 5 katika mechi 5 mfululizo za CL na sasa anakuwa mchezaji wa kwanza wa As Roma kuwahi kufunga mabao 5 katika michezo 5 mfululizo ya klabu hiyo katika Champions League.

Lakini pia bao la Edin Dzeko linamfanya kuifikia rekodi ya Samuel Etoo ya mchezaji wa klabu toka Italia kuwahi kufunga mabao 8 katika Champions League, rekodi aliyoweka mwaka 2010/2011, Radja Nainggolan alifunga mabao mengine mawili kwa As Roma.

Visit website
 
Back
Top Bottom