Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mtoto anapozaliwa huwa kunakuwa na dhana nyingi juu yake ikiwamo imani kuwa kitovu kikimdondokea sehemu za siri husababisha ugumba kwa wa kike na ukosefu wa nguvu za kiume kwa wa kiume.

Wanawake wengi huambiwa hayo na wazazi wao mara baada ya kujifungua.
 
Marina Haule, mkazi wa Dodoma anasema: “Ni mila tu ambayo mama yangu aliniambia na nikawa makini kweli kwa sababu niliogopa mtoto wangu kuwa si mwanaume kamili lakini sijui kwa undani inasababishwa na nini.”

Wanawake wengi hurithishwa na kizazi hata kizazi. Mkunga wa jadi kutoka Kijiji cha Chikunja wilayani Masasi, Zainab Chiuta anasema hata wao walifundishwa hivyo na bibi zao na kila wanapomzalisha mwanamke humpa maagizo hayo.
 
Ni imani tuliyorithi kuoka kwa wazazi, kwa sababu imekuwapo basi tunaendelea nayo na kimsingi tunaamini ni kweli,” anasema

Anasema si hivyo tu hata kitovu chenyewe kikishaanguka, hakitupwi ovyo bali kinachimbiwa ardhini au kwenye majivu.

“Kimila, kitovu hakitupwi tu, kinazikwa ili kuepusha mtu kumdhuru mtoto. Kitovu kina mambo mengi,” anasema
 
Back
Top Bottom