Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mkurugenzi mtendaji wa kliniki ya kimataifa ya afya ya uzazi kwa baba, mama, mtoto na vijana (AMM), Dk Ali Mzige anasema hizo ni dhana potofu ingawa kitovu kinatakiwa kulindwa kukiepusha na bakteria.

“Hizo cha mtoto kinatakiwa kilindwe kisiingie uchafu kwani bakteria wakiingia wanaweza kusababisha homa kali na maradhi mengine. Hilo ni jambo la hatari,” anasema
 
Anasema zamani kitovu kilifungwa na kamba lakini siku hizi kinafungwa na kifaa maalum na kitovu huanguka chenyewe.

“Kikianguka popote pale, mtoto wa kiume ataendelea kuwa wa kiume na wa kike ni wa kike labda kama ana shida katika fumo wa homoni,” anasema.

Ni vizuri mama akawasiliana na wakunga mara kwa mara kuhusu maendeleo ya mtoto hasa kama kitovu cha mtoto kinatoa harufu au damu.
 
Mtaalamu huyu wa afya ya mama na mtoto amezungumzia pia suala kitovu cha mtoto kuwa kikubwa na kusema hurudi na kuwa katika hali ya kawaida katika umri wa miaka mitatu hadi minne.

“Lakini kama hakijarudi hadi umri wa miaka minne, mtoto anaweza kufanyiwa upasuaji mdogo tu ambao hukirudisha kuwa katika hali ya kawaida,” anasema

Mtaalamu wa Afya kutoka Hospitali ya Bugando, Dk Kanaani, amesema hakuna ukweli wowote kisayansi kuhusu hilo bali ni dhana inayoenezwa na wakunga wa jadi au wakunga walioajiriwa katika sekta rasmi.
 
Hakuna tafiti za kisayansi kuhusu hilo, kwa uzoefu wangu, sijawahi kuona uhusiano kuhusu kitovu na sehemu za siri za mtoto,” anasema

Dk Kanaani anasema ugumba kwa wanawake au wanaume, huweza kumpata mtu ukubwani au kwa kuzaliwa nao na sio kwa kuangukiwa kitovu.

“Labda na sisi kama wanasayansi tusilidharau hili tulifanyie utafiti, lakini mpaka sasa hakuna uhusiano,” anasema
 
Mwanasaikolojia wa jijini Dar es Salaam, Josephine Tesha anasema hakuna ukweli wowote katika hilo.

“Ukiamini sana hivyo vitu, unaweza kuathirika kisaikolojia. Ikatokea kweli kitovu kikadondokea sehemu za siri za mtoto, kimsingi mzazi anaathirika kifikra,” anasema
 
Magonjwa ya afya ya akili yanaendelea kuitesa jamii huku baadhi yake yakiangukia kwenye unywaji wa pombe kupita kiasi, uvutaji bangi na matumizi ya dawa nyingine za kulevya.

Wataalamu wa afya wamebaini kuwa siyo watu wote wanaovuta bangi na kunywa pombe kupita kiasi hupenda kufanya hivyo, wengine hulazimika kutokana na maradhi ya afya ya akili.
 
Mtaalamu wa kitengo cha afya ya akili wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Saidi Kuganda anasema maradhi hayo yanaweza kumsababisha mtu kutumia mihadarati na kunywa pombe.

“Unajua akili inapopata shida mhusika husikia kelele kichwani na hutafuta mbinu za kukabiliana na hali hiyo. Akibaini akinywa pombe hatazisikia, basi hukimbilia kunywa na akibaini kuwa akivuta bangi hatasikia karaha au usumbufu anaoupata, basi atakuwa anavuta na atafanya hivyo kila anapohisi kupata shida hiyo,” anasema Kuganda.
 
Anasema mara nyingi wanaume ndiyo hukimbilia mbinu hizo ukilinganisha na wanawake ambao wengi wao hufikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Dk Kuganda anafafanua maana ya magonjwa ya afya ya akili na kusema, ni yale yanayoathiri uwezo wa mtu kufikiri, kuhisi, kutambua na kutenda katika utashi wake.
 
Hivyo mgonjwa anakuwa na tabia au mwenendo ulio tofauti au usioendana na jamii husika kiimani, kimila na desturi,” anabainisha mtaalamu huyo.

Anasema ikitokea mtu amevuta bangi ikamchanganya akili akafikishwa hospitalini akiwa amefungwa kamba hukaa naye akipatiwa huduma ya kwanza hadi pale nguvu ya bani itakapokwisha.
 
Kama ni mvutaji wa kawaida nguu ya bangi ikiisha anakuwa sawa na anaruhusiwa kurudi nyumbani na jambo hilo ni kawaida kabisa, lakini akiwa anavuta kwa sababu ya matatizo ya akili hata nguvu ya bangi ikiisha anakuwa hayupo sawa na hafanyi vitu vya kawaida, ”anasema.

Mtaalamu huyo anasema bahati mbaya ni asilimia 40 ya watu wenye maradhi hayo hufikishwa hospitali, tofauti na hapo unyanyapaa husababisha wengi wao kukimbia na kuingia mitaani.
 
Kauli ya Dk Kuganda inaungwa mkono na makala iliyochapishwa kwenye jarida lijulikanalo kama Journal American Psychiatry la nchini Marekani, iliyoeleza kuwa matumizi ya pombe na dawa za kulevya mara nyingi hutumiwa kukabiliana na hali mbalimbali za afya ya akili, ikiwa ni pamoja na kutojitambua.
 
Watu wengi wanaopata shida ya maradhi ya akili hushindwa kukabiliana nayo na hutafuta liwazo la hali hiyo, mwisho huangukia katika matumizi ya pombe na dawa za kulevya,” anasema mtaalamu wa afya, Dk Robert Freedman.

Freedman ambaye ndiye mhariri mkuu wa jarida hilo, anasema hata hivyo siyo kila anayekunywa pombe na kutumia dawa za kulevya anakuwa anapigana na matatizo ya akili, “Wapo wanaotumia kwa utashi wao tu,” anasema.
 
Back
Top Bottom