Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Nchi nyingine inayoamua kuchukua uamuzi wa kusitisha shughuli za mashirika ya utangazaji ya kimataifa ni Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DR Congo) kutokana na uhusiano baridi na Radio France International (RFI) na Radio Okapi inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
 
Burundi iko kwenye kampeni ya kuhamasisha wananchi kushiriki kupiga kura ya maoni kuunga mkono au kupinga mabadiliko ya katiba ambayo yanalenga kuongeza mihula ya rais. Ikiwa kura ya ‘ndiyo’ itashinda Mei 17 Rais Pierre Nkurunziza ataendelea kusalia madarakani.
 
Kadhalika kura hiyo ya maoni itaongeza muhula mmoja kutoka miaka mitano kuwa saba na Nkurunziza ataruhusiwa kuwania tena mwaka 2020. Kwa katiba hiyo mpya rais atakaa mamlakani kwa vipindi viwili vya miaka saba saba, na haitaangalia vipindi vya nyuma hivyo ataweza kutawala hadi mwaka 2034.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…