Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Bruce Grobbelaar

(Liverpool 1983/84)

Kipa wa huyu wa kimataifa wa Zimbabwe mzaliwa wa Afrika Kusini anaingia katika rekodi hii kuwa mchezaji wa kwanza kutoka Bara la Afrika kutwaa taji hilo. Alikuwa nguzo katika fainali kati ya timu yake Liverpool dhidi ya AS Roma katika pambano la fainali msimu wa 1983/84 huku Liverpool ikishinda kwa penalti 4-2. Grobbelaar alisifika vilivyo kama chanzo cha wachezaji wa Roma kukosa penalti kutokana na tabia yake ya kutingisha miguu ovyo wakati akiwa langoni.
 
Rabah Madjer (Porto 1986/87)

Staa wa pili wa Afrika kuchukua klabu bingwa ya Ulaya huku akiwa mchezaji wa kwanza mwenye asili ya Kiarabu kutoka Afrika kutwaa taji hilo kama Salah anavyotaka kufanya mwaka huu. Alijiunga na Porto msimu mmoja kabla ya mafanikio haya na kufanya kazi nzuri wakati Porto ikiichapa Bayern Munich mabao 2-1 msimu wa 1986/87 na kutwaa taji lake la kwanza la ubingwa wa Ulaya.
 
Madjer alifunga bao la kusawazisha dakika ya 77 kabla ya staa mwingine, Juary kufunga bao la pili dakika chache baadaye.

Abedi Pele Ayew (Marseille 1992/93)

Kiungo wa kimataifa wa Ghana ambaye ni baba wa mastaa wa sasa wa Swansea City na Timu ya Taifa ya Ghana, Andre Ayew na Jordan Ayew. Anakuwa mchezaji wa tatu kutoka Bara la Afrika kutwaa taji hili.

Alikuwa mchezaji bora wa mechi katika pambano la fainali kati ya timu yake Marseille dhidi ya AC Milan mwaka 1993. Alipiga kona ambayo iliunganishwa na mshambuliaji, Basile Boli na hivyo kuipa Marseille ubingwa huo.
 
Eti
IMG-20180504-WA0019.jpg
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hongera mkuu sisi tunabugia fikra tu
Hahah!! Unatakiwa kufanya kweli sasa mkuu
 
Back
Top Bottom