Zifuatazo ni faida nane tu za kufunga kiafya:
1. Husaidia kupunguza uzito wa mwili
Tafiti zinaonesha kuwa, kufunga kwa vipindi vifupi kunaongeza ufanisi wa mfumo wa mwili kutumia maji na chakula unachokula (metabolism) kwa asilimia kati ya 3.6 hadi 14 ikiusaidia mwili kuchoma kalori zaidi. Kwa sababu hiyo, funga inakusaidia sio tu kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, bali husaidia pia kupunguza kiasi cha chakula unachokula na hivyo kupunguza uzito wa mwili.