Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

3. Huimarisha kinga ya mwili
Kuondoa sumu mwilini na kupunguza wingi wa mafuta mwilini unapofunga inasaidia kuimarisha kinga ya mwili. Pia, ukiwa unakula mlo kamili katika kipindi cha mfungo kama kula matunda kwa wingi wakati wa kufungua inauongezea mwili uwezo wa kuhifadhi vitamini na madini muhimu ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
 
4. Husaidia ulaji bora
Funga hupunguza tamaa za kula hovyo vyakula visivyo na ubora kiafya na huongeza hamu ya kula mlo sahihi hasa maji na matunda. Hii husaidia ulaji sahihi hata baada ya kipindi cha mfungo kupita.
 
5. Kuboresha afya ya ubongo
Funga inasaidia kuimarisha mifumo mbalimbali ambayo inajulikana kwa kuboresha afya ya ubongo. Husaidia sana kuongeza seli mpya za mfumo wa neva za fahamu ambazo zina faida kubwa katika ufanyaji kazi wa ubongo na huulinda kutokana na madhara mbalimbali.
 
Zaidi ya hapo, funga inaupa changamoto mpya ubongo wako na kuufanya uweze kukabiliana na hali ambayo haikuizoea jambo linalosaidia kupambana na maradhi kwa haraka sana. Pia funga inasaidi kuepuka magonjwa ya kupooza kama Alzheimer’s na Parkinson’s na kwa wakati huo huo kusaidia kuimarisha uwezo wa kumbukumbu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…