Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

HALI YA HEWA
Nyanya chungu za aina zote hustawi sana sehemu yenye jua na udongo wenye kupitisha maji vizuri na udongo wenye pH kati ya 5.5 na 6.8. Gilo ni aina ambayo hustawi sana kwenye joto la mchana ni kati ya 25°C na 35°C (77°F na 95°F). Kumba ni aina hustawi maeneo yenye joto sana la 45°C na unyevu kidogo, Shum ni aina inahitaji joto na unyevu ili kustawi. Hakuna aina ya Nyanya chungu inayovumilia kwenye baridi kali na hali ya majimaji.
 
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Lima shamba lako vizuri kwa kutumia trekta, jembe la ng’ombe, jembe la mkono au pawatila, hakikisha shamba linakuwa halina nyasi, changanya samadi au mboji na udongo ili kuongeza rutuba.
 
UTAYALISHAJI WA MBEGU
Mbegu za nyanya chungu zinauzwa kutoka baadhi ya makampuni ila kuna njia ya kupata mbegu kutoka kwenye tunda. Chukua nyanya chungu iliyokomaa menya vizuri baada ya hapo kusanya mbegu zilizopo ndani ya tunda, baada ya hapo ziweke kwenye kipande cha karatasi ili zikauke katika sehemu isiyopitisha mionzi ya jua ya moja kwa moja.
 
Mbegu zikisha kauka zinaweza kutunzwa kwa miaka mingi na kuendelea kutumika. mbegu lazima zioteshwe kwenye kitalu cha sentimita 15 (6 inch) au zaidi 20 cm (8 inch) ya safu. miche kutoka kitaluni inakuwa tayari kupandwa ikifika urefu wa sentimita 15 mpaka 20 (6–8 inch) na iwe na majani 5–7. Mmea inatakiwa uwe na nguvu katika mashina na yenye nafasi ya sentimita 50 (20 inch) mbali ruhusu sentimita 75 (30 inch) ya safu.
 
UPANDAJI
Kutoka kwenye kitalu miche ifikiapo kimo cha sentimeta 15 hadi 20 au majani manne 5-7 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50 kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya “Ngogwe” hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.
 
MAGONJWA &WADUDU
Nyanya chungu ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa
yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara yake si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
 
UVUNAJI
Nyanya chungu huvunwa wakati zikiwa bado mbichi, hukomaa baada ya siku 100 mpaka 120 kutoka kupandwa, unashauriwa uvune kabla hazija badilika rangi . Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.
 
Zifuatazo ni faida nane tu za kufunga kiafya:

1. Husaidia kupunguza uzito wa mwili
Tafiti zinaonesha kuwa, kufunga kwa vipindi vifupi kunaongeza ufanisi wa mfumo wa mwili kutumia maji na chakula unachokula (metabolism) kwa asilimia kati ya 3.6 hadi 14 ikiusaidia mwili kuchoma kalori zaidi. Kwa sababu hiyo, funga inakusaidia sio tu kuboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, bali husaidia pia kupunguza kiasi cha chakula unachokula na hivyo kupunguza uzito wa mwili.
 
2. Inapunguza uwezo wa mwili kuzuia insulin
Funga inasaidia mwili usizuie insulin jambo linalosababisha kupunguza kiwango cha sukari mwilini. Zaidi ya hilo, funga husaidia kuongeza mmeng’enyo wa sukari jambo linalosaidia kuufanya mwili kuwa na nguvu zaidi. Kupungua kwa kuzuiwa insulin inasaidia kupunguza harati za kupata ugonjwa wa kisukari aina ya pili (type 2 diabetes).
 
3. Huimarisha kinga ya mwili
Kuondoa sumu mwilini na kupunguza wingi wa mafuta mwilini unapofunga inasaidia kuimarisha kinga ya mwili. Pia, ukiwa unakula mlo kamili katika kipindi cha mfungo kama kula matunda kwa wingi wakati wa kufungua inauongezea mwili uwezo wa kuhifadhi vitamini na madini muhimu ambavyo vyote kwa pamoja husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
 
5. Kuboresha afya ya ubongo
Funga inasaidia kuimarisha mifumo mbalimbali ambayo inajulikana kwa kuboresha afya ya ubongo. Husaidia sana kuongeza seli mpya za mfumo wa neva za fahamu ambazo zina faida kubwa katika ufanyaji kazi wa ubongo na huulinda kutokana na madhara mbalimbali.
 
Back
Top Bottom