Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Venus ni sayari yenye volcano nyingi kuliko sayari yeyote katika mfumo wa jua ,kuna aina 1600 za volcano katika safari ya venus….venus ni sayari yenye anga chafu kuliko sayari yeyote katika mfumo wa jua uku ikiwa imetawaliwa na gesi chafu ya carbon dioxide ,aisee uko kikianzishwa kiwanda cha coca cola watapata faida sana maana carbon dioxide ni bure. Pia kutokana kuwa na anga chafu inakuwa ni vigumu sana kuifanyia uchunguzi sayari hii ambapo wana astronomia wanashindwa kuitazama sura yake vizuri kwakutumia telescope kutoka duniani.
 
Ni sayari inayo ng’aa sana katika mfumo wa jua huwa inaonekana muda mfupi baada ya jua kuzama upande wa magaribi, huwa inaonekana katika nyuzi 45. Pia asubui inakuwa ya mwisho kupotea baada ya nyota zote kupotea na huwa ina ng’aa sana ndiyo maana ikaitwa ZUHURA.
 
Ukizipanga sayari zote nane katika sayari zinazoweza kusuport life basi venus itakuwa ya mwisho kutokana na kuwa na hewa nyingi sana ya ukaa yaani carbon dioxide na gesi zingine nyingi chafu pamoja na vimbunga vingi na volcano zinazolipuka muda wote
 
Venus ina carbon dioxide nyingi katika anga lake na pia volcano kila kona na hii upelekekea sayari kuwa na joto kali sana kuliko sayari zote hata ile ya Mercury (Zebaki)ambayo ndio iko karibu na Jua.
 
Pia inakisiwa kuwa miaka ya mwanzoni (kati ya bilioni 3 na miaka milioni 600 iliyopita) wa kuwepo kwa uhai duniani, anga la Venus ilikuwa ni kama la dunia kabla haijachafukwa na hewa ya ukaa kama ilivyo sasa na kwa hiyo inakisiwa pia kuwa kuna kila dalili kuwa kulikuiwa na uhai mdogo kwenye baadhi ya maeneo hapo zamani.
 
NB: Urusi lilikuwa taifa la kwanza kutuma chombo kwenda sayari ya Venus miaka iyo ya 1970’s lakin vyombo vingi vilikuwa vikiungua kabla ata ya kufika lakin ata vyombo ambavyo vilifika vili tuma picha hafifu mda mfupi kabla ya kuungua kutokana na joto lililopo katika venus lakin miaka ya mbeleni urusi na Marekani walifanikiwa kufanya mission za kutuma vyombo katika sayari iliyo karibu na dunia kwa ajili ya kuichunguza Venusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…