Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Cristiano Ronaldo amezua hofu baada ya kuumia kifundo cha mguu na kulazimika kupumzishwa wakati wa mapumziko wa mchezo wa El Clasico uliomalizika kwa sare 2-2 kati Barcelona na Real Madrid.

Mshambuliaji huyo Mreno alionekana akipatiwa matibabu katika kipindi cha kwanza jambo lililomfanya Kocha Zinedine Zidane kumpumzisha.
 
Taarifa zinasema Ronaldo amepata maumivu ya kawaidi ya kifundo cha mguu na Zizou kumpumzisha ilikuwa ni mbinu ya kuepisha matatizo zaidi.

Ronaldo aliumia baada ya kufunga bao la kwanza kwa Real Madrid kwenye Uwanja wa Nou Camp baada ya hapo alipatiwa matibabu nje kabla ya kurudi uwanjani.
 
Real Madrid itawavaa Liverpool katika fainali ya Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa mwezi huu, kabla ya kuelekea katika Kombe la Dunia.

Zidane alisema: "Ronaldo amepata maumivu kidogo. Tunasubiri kupata majibu ya vipimo kutoka kwa madaktari, hakuna wasiwasi kama hatoweza kucheza Kiev, lakini nasema ni jambo dogo.

"Kwa sasa hayupo vizuri, lakini ni dogo. Tunasubiri hadi taarifa ya madaktari itakapotoka."
 
Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos amemshutumu Luis Suarez, kwa kusema timu yake iligoma kusimamisha mchezo baada ya mshambuliaji huyo wa Barcelona kumia kwa sababu "tabia yake ilivyo".

Mechi nyingine ya Clasico ilimalizika kwa sare 2-2, kwenye Uwanja wa Camp Nou jana Jumapili huku Barcelona ikiwa katika mstari mzuri wa kumaliza msimu wa LaLiga bila ya kufungwa.
 
Lakini Madrid walijikuta katika wakati mgumu kwa kukataa kutoa mpira nje baada ya Suarez kumia wakati walipokuwa wakijaribu kutafuta bao la ushindi.

Hata hivyo, Ramos hakujutia kitendo hicho kutokana na historia ya mshambuliaji huyo wa Uruguay alikuwa na lengo la kusimamisha mchezo.
 
Yeyote ambaye angeumia na utongeona kuwa ameumia kweli, tungetoa mpira," alisema Ramos.

"Tungefanya hivyo kwa heshima yake.

"Lakini tunajua jinsi alivyo, aina yake ya uchezaji na jinsi tabia yake ilivyo, sikudhani ni muhimu kwetu kufanya hivyo kwake."
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…